Sheria kali iliyokuwa imepitishwa ilisababisha jamii ya kimataifa kuinyima Uganda msaada
Suala la wapenzi wa jinsia moja na sheria nchini Uganda baado linazua mijadala nchini humo.
Miezi mitatu tangu mahakama nchini humo kuibatilisha sheria dhidi ya ushoga kwa sababu za kiufundi sasa habari zingine zimeanza kujitokeza kuhusu uwezekano wa serikali kuleta tena muswada huo bungeni.
Kujitokeza tena kwa suala hilo wakati huu ni baada ya hati maluum kuvujishwa . Hati hiyo ya kurasa tano ni ya muswada jaribio kuhusu suala la mapenzi ya watu wa jinsia moja.
Hati hiyo inaitwa : 'Mswada wa mwaka 2014 kuzuia kueneza visa vya kujamiiana ambavyo si asili wa mwaka wa 2014.
Katika hati hiyo kuna pendekezo la kifungo cha miaka saba ikiwa mtu atapatikana na hatia ya kile kinachoweza kuitwa kufagilia ushoga.
Neno lilotumiwa ni kutangaza na hivyo kutiliwa mkazo badala ya sheria ya zamani iliokuwa inatilia mkazo ushoga wenyewe.
Wachambuzi wanasema kuwa hati hii ikipasishwa kama sheria itakuwa mbaya zaidi ya ile iliobatilishwa kwani itawahukumu watu wengi mkiwemo vyombo vya habari pamoja na watu wote wanaotumia mitandao yote ya kijamii.
'Sheria mbadala kali zaidi?' Maandamano yalifanyika Uganda kumunga mkono Rais kwa kupitisha sheria kali dhidi ya ushoga
Hati hii inasema kuwa mtu yeyote akipatikana na hatia atahukumiwa kifungo cha miaka saba.
Sheria iliobatilishwa na mahama mapema Agosti mwaka huu miongoni mwa mengine ilikuwa inasema yeyote akipatikana na hatia atafungwa jela maisha.
Waziri wa taifa wa sheria na naibu mwanasheria mkuu Fred Ruhindi akizungumza na BBC kwa simu amek
ataa kutoa kauli kwa kile alichoita hati iliovujishwa na kusema kuwa mchakato kuhusu sheria mpya ya kudhidbiti ushoga unaendelea.
Yeye waziri anaehusika na maadili Padri Lokodo amesema hajui lolote kuhusu hati hiyo.
Hatua zilizofuata
Yeye waziri anaehusika na maadili Padri Lokodo amesema hajui lolote kuhusu hati hiyo.
Hatua zilizofuata
0 comments:
Post a Comment