Lengo ni kuruhusu wananchi kutoka nchi moja kwenda kufanya kazi nchi nyingine bila kuwapo na masharti magumu.
Arusha. Serikali za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeshauriwa kuondoa vikwazo vya ajira kwa walimu wa masomo ya Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili ili kusaidia kukuza sekta ya elimu kwa nchi wanachama.
Wito huo ulitolewa na Profesa Kitila Mkumbo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakati wa tamasha la asasi za kiraia kwa nchi za Afrika ya Mashariki, mkoani hapa.

Alisema katika nchi zote wanachama kuna uhaba wa walimu, hivyo ni muhimu kushirikiana.
Profesa Mkumbo alisema Kenya kuna walimu wa kutosha wa Kiingereza, lakini hakuna walimu wa kutosha wa Kiswahili na Kifaransa, wakati Tanzania ina walimu wa kutosha wa Kiswahili, lakini kuna upungufu wa walimu wa Kiingereza na Kifaransa.
Alifafanua kuwa Uganda ina walimu wa kutosha wa Kiingereza, lakini hakuna walimu wa kutosha wa Kifaransa na Kiswahili, huku Rwanda na Burundi zikiwa na walimu wa kutosha wa Kifaransa, lakini hazina walimu wa Kiingereza na Kiswahili.
“Mazingira haya yanaonyesha ni muhimu kuondolewa vikwazo vya ajira kwa walimu katika nchi husika,” alisema Mkumbo.
Alisema changamoto nyingine kwenye jumuiya ni viongozi wa siasa kutanguliza mbele masilahi ya nchi zao kuliko ya jumuiya.
“Lazima turejee kujenga jumuiya hii, siyo kila nchi kutetea masilahi yake ndani ya jumuiya,” alisema.
Alisema utamaduni wa baadhi ya viongozi wa siasa kuangalia zaidi masilahi ya upande wao bila kujali fursa zingine kutoka kwa majirani zao, unapaswa kuachwa mara moja.
Katika tamasha hilo lililohusisha mashirika zaidi ya 200 kutoka nchi zote za Afrika Mashariki, yalipitishwa maazimio ya kuimarisha uhusiano wa asasi hizo ili kuibua fursa ndani ya jumuiya.
Mwananchi.
0 comments:
Post a Comment