2015-01-31

Shocking VIDEO: Ona kilichomkuta rapa baada ya kumwinamisha dansa wake akiwa stejini...

Rapa wa Muziki wa kizazi kipya, alijikuta katika wakati mgumu akiwa stejini na dansa wake baada ya kumwinamisha wakicheza. 

Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa washabiki ambao walikuwa wakishangilia kwa furaha lakini hali ilipobadilika kilichotokea dada yule hakuna cha shabiki wala rapa aliyevumilia.

Jionee video hii iliyorekodiwa hapo KICC

Zuma; licha ya changamoto hizo, Bara la Afrika linapiga hatua kimaendeleo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisoma makabrasha ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU unaofanyika kwa siku mbili jijini Addis Ababa kuanzia leo. Nyuma ya Mhe. Rais ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb). Waziri wa Jinsia na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Sophia Simba (Mb) na Balozi wa Tanznia nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz (mwenye ushungi).




Wakuu wa Nchi za Afrika wamekumbushwa kuwa, Mwaka 2015 umeingia lakini Bara la Afrika bado linakabiliwa na changamoto nyingi ambazo kama hazitapatiwa ufumbuzi ustawi wa bara hilo utaendelea kudumaa. Kauli hiyo ilikuwa inarudiwa mara kwa mara na viongozi waliopata fursa ya kuhutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa siku ya Ijumaa tarehe 30 Januari 2015.
Changamoto hizo ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi, ugaidi, migogoro ya kutumia silaha, ukatili wa kutisha, biashara haramu ya binadamu, umasikini na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Walishauri katika mwaka wa 2015 lazima matatizo hayo yajadiliwe kwa kina kwa madhumuni ya kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu.

Alipokuwa anahutubia mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Nkosazana Zuma alisema kuwa, licha ya changamoto hizo, Bara la Afrika linapiga hatua kimaendeleo na kwamba Agenda 2063 inayowasilishwa katika Mkutano huo inatoa wito kwa Serikali na sekta nyingine kushirikiana kwa pamoja ili kukuza uchumi kwa kuweka mkazo kwenye ubunifu katika sekta ya kilimo, usindikaji wa mazao na ujenzi wa miundombinu.

Mhe. Zuma alisisitiza umuhimu wa kutumia fedha za ndani kwa ajili ya kugharamia miradi ya kipaumbele ambayo imezingatiwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka 10 ambao nao utawasilishwa katika mkutano huo. Alieleza kuwa Sekretarieti imefanyia kazi pendekezo la kutafuta vyanzo mbdala vya fedha ambapo Mawaziri wa Fedha walijadili na ripoti yao itawasilishwa wakati wa mkutano huo. Umoja wa Afrika pia umeanzisha Mfuko Maalum utakaozinduliwa wakati wa mkutano huo kwa ajili ya kuhifadhi fedha hizo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Ban Ki-moon alieleza kuwa mwaka 2014, AU na UN zilishirikiana kutafuta amani katika nchi zenye migogoro. Alisema mafanikio makubwa yalipatikana na hivyo kusisitiza kuwa pande zilizosaini mikataba ya amani lazima zitekeleze vipengele vya mikataba hiyo. Alitoa mfano wa Mkataba wa Arusha na kusema kuwa pande zinazohusika zitekeleze makubaliano ya kugawana madaraka. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kukitokomeza kikundi cha waasi cha FDLR kinachoendesha uasi wake Mashariki mwa DRC.
Mhe. Ban Ki-moon pia aliwakemea viongozi wa Afrika wanaong’ang’ania madaraka. Aliwashauri viongozi hao waache tabia hiyo na kuruhusu demokrasia ichukue mkondo wake.
Rais wa Kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Sam Kutesa pamoja na mambo mengine, alizungumzia mabadiliko ya mfumo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Alisema katika uongozi wake atafanya jitihada kuhakikisha kuwa mfumo wa Baraza hilo, chombo ambacho alikitaja kama kisichokuwa na demokrasia kuliko vyombo vyote duniani unafanyiwa mabadiliko.

Viongozi hao pia walihimiza juhudi za kutafuta tiba na chanjo ya ugonjwa wa Ebola na kusisitiza kuwa kampeni ifanywe ili nchi zilizoathirika na ugonjwa huo zisamehewe madeni.


SWALI: Licha ya changamoto bara gani linapiga hatua kimaendeleo

a. AFRIKA
b. Chile
c. TWIGA

Kujibu swali hili ujishindie muda wa maongezi na kuwa mfukuaji wa fukufuku bora kwa wiki bofya hapa

Mtaalamu wa silaha za kemikali IS auwawa

Mlipuko

Jeshi la Marekani linasema kuwa mtaalamu mmoja wa silaha za kemikali aliyekuwa akifanya kazi na kundi la Islamic State ameuawa kwenye mashambulizi ya muungano nchini Iraq.
Marekani inasema kuwa kifo cha mwanamume huyo kwa jina Abu Malik kitavuruga uwezo wa kundi hilo wa kuunda na kutumia silaha za kemikali.

Abu Malik anaripotiwa kufanya kazi kama mtaalamu wa silaha za kemikali kwa rais wa zamani wa Iraq Sadam Hussein kabla ya uvamizi ulioongozwa na Marekani mwaka 2003.

Kundi la Islamic State hudhibiti maeneo makubwa nchini Syria ambapo serikali imekuwa ikiharibu silaha za kemikali.

Chenge Ageuka Mbogo Bungen.Amtaka Halima Mdee Atoe Ushahidi



MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) ametakiwa kuwasilisha ushahidi kuthibitisha kauli yake ya kumtuhumu Mbunge Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM), kwa ufisadi. 


Chenge alilazimika kuomba utaratibu wa kiti juzi, baada ya Mbunge huyo wa Kawe kumtaja mara mbili wakati akichangia mjadala wa taarifa za kudumu za Bunge zilizowasilishwa juzi.

Mara ya kwanza, Mdee alimhusisha Chenge na mkataba mbovu wa Kampuni ya Ndege (ATCL) uliosababisha Serikali kuingia hasara ya zaidi ya Sh bilioni 90.

Licha ya kumtaja kwenye ufisadi huo ambao kwa mujibu wa Mdee, Chenge ndiye alikuwa Waziri wa Wizara yenye dhamana na ATCL, pia alimtaja kuhusika katika kashfa nyinginezo ikiwemo suala la utoaji takribani Sh bilioni 200, katika iliyokuwa Akaunti ya Tegeta Escrow ya Benki Kuu (BoT).

“Wabunge tuanze kuchunguzana humu ndani na kushughulikiana,”alisema Mdee na kutaja kwamba kwa kuanza, waanze na Chenge pamoja na Dk Shukuru Kawambwa (Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi), akimhusisha kuwa aliwahi kushika wizara hiyo yenye dhamana na ATCL.

Kauli hiyo ilimfanya Chenge kusimama na kusema; “kwa heshima zote nimemvumilia sana mheshimiwa (Mdee) anayechangia hoja hii. Kama ana ushahidi wa hayo anayosema, kanuni zetu zinatutaka ayawasilishe mbele yako.

“Mimi ningelipenda Bunge hili liendelee kuwa na heshima yake. Pili naomba sana, hayo wanayoyasema wawe na ujasiri wa kwenda kuyasemea nje ya ukumbi huu wa Bunge, wasijifiche kwenye kinga ya Bunge.

“Nina mengi ya kusema, lakini kwa sababu nimesimama kwa hoja ya utaratibu, kunitaja moja kwa moja, naomba aweke hoja mezani,”alisema Chenge.

Mwenyekiti wa Bunge alikubaliana kwamba Mdee awasilishe ushahidi kwa kiti. Hata hivyo Mdee alijibu, “Kuna utaratibu wa kikanuni, vielelezo nikitakiwa kuleta nitaleta.

"Tunazungumza hapa matumizi mabovu, mikataba mibovu na wizi wa mali ya umma. Mzee wangu (Chenge) ni rafiki yangu lakini nimeamua nimfungukie kwa sababu haya ni mambo makubwa.”
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...