2015-01-30

Huo Ndio;Ukweli Kuhusu Tevez Aliyekatwa Uume Wake Baada ya Kuwazulumu Madawa ya Kulevya Wenzake


HABARI ZA UHAKIKA JUU YA SAKATA LA JUMAANNE TEVEZ. Nikweli kwamba huyu bwana yuko South Africa Pretoria. Bwana Tevez alodhaminiwa mzigo na vijana 
wenzake huko Bondeni kwamba akauze kisha alete Mpunga. Mdhamini alikuwa ni Kijana wa Kibongo anayeonekana pichani anayeitwa Jeff Katili mtoto wa Ilala ambaye maskani yake ni South. TEVEZ baada ya kuchukua mzigo uliokuwa na thamani ya takriban milioni mia moja na hamsini (150,000,000/=) aliingia mitini hakurudi tena. Kilichotokea Jeff baada ya kubanwa na wana akawaambia kuwa tulieni nitamleta tu.


Basi Jeff akamrubuni Tevez kuwa njoo Kuna kazi.. Tevez akaingia mzima mzima akaenda hadi Pretoria wiki iliyopita na kufikia kwa Jeff Katili na kupata mapokezi mazuri kama kawaida. Baada ya kufika walitoka kwenda matembezi 
KWAZULU NATAL... wakiwa huko walifikia kwa washkaji zao wa kibongo lakini kwenye nyumba ambayo ilikuwa kama holi haina chochote ndani. Chini lilitandikwa karatasi la nailoni ili kuepusha damu isitapakae. Alibanwa juu ya mzigo na mtesaji mkubwa alikuwa Jeff Katili mwenyewe ambaye ni mdhamini. Tevez hajang'olewa jicho bali alipigwa Ngumi hadi jicho likaenda ndani... NGUMI YA MTOTO WA KIUME.

Ameteswa sana na amekatwakatwa na viwembe mwili mzima. Zakari yake haijakatwa kama picha zilivyoonyesha bali imekatwa na viwembe. Taarifa zilitumwa kwa kaka yake na akina Jeff na kuwataka watume pesa la sivyo wanamuua. familia kupitia kaka yake imeshatuma pesa nusu na sas anatibiwa hukohuko South na atarejea punde. Uzushi kuwa amekufa hauna ukweli na hizi ni habari kamili kutoka kwa watu wa karibu na familia hiyo. GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...