2015-01-05

KUME KUCHA;MUME MCHEPUKO WAGOMBEA MTOTO HADHARANI!


Mwanamke, Bahati Ramadhani anayeidaiwa kumgonganisha mumewe na mchepuko. 
 

Makubwa! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mke wa mtu aliyekuwa akiishi ukweni na mumewe wa ndoa, Bahati Ramadhani, amenusurika kuuawa na ndugu wa mumewe wakiwemo mawifi na wakwe zake baada ya kudaiwa kumgonganisha mumewe na mchepuko wake na kujikuta wakigombea mtoto. 

Tukio hilo la kushangaza lililojaza kadamnasi lilijiri nyumbani kwa wakwe hao, Mtaa wa Mawenzi jirani na Soko la Matunda la Mawenzi la mjini hapa wiki iliyopita ambapo Bahati alikuwa akiishi na mumewe, ldd Yusuf.
Ilielezwa kwamba wanandoa hao walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume (jina kapuni) ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 2.

Polisi akimbana kwa maswali mwanamke huyo kuhusu utata uliotokea. Siku ya tukio, mama mkwe wa Bahati, Faidha Cosmas alishtukia dili baada ya kuona sms ya mwanaume ‘aliyeseviwa’ kwa jina la Saddy kwenye simu ya Bahati ikimweleza kwamba alikuwa amemtumia fedha za matumizi ya mtoto wao huyo.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...