2015-02-20

JOHARI ATUBU KUMPORA RAY KWA MAINDA...............soma hapa kilichojiri

 
 STAA wa sinema za Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amekiri kwamba wakati anaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na nyota wa fani hiyo, Vincent Kigosi ‘Ray’ alijua yupo na nguli wa filamu, Ruth Suka ‘Mainda’. 


          Staa wa sinema za Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.

Katika mahojiano mafupi na gazeti hili yaliyofanyika Jumanne iliyopita jijini Dar, hali ilikuwa hivi:
Ijumaa: “Kwanza napenda kujua kama kweli umerudiana na Ray maana kuna minong’ono kwamba penzi lenu kama zamani.”

Johari: “Siyo kweli. Kwanza mimi sipendagi hayo maswali miaka yote mambo ni hayohayo, sasa nimekua mtu mzima na mambo lazima yabadilike.”
Ijumaa: “Kwa hiyo huna uhusiano na Ray?”
Johari: “Sina.”


            Nguli wa filamu, Ruth Suka ‘Mainda’.

Ijumaa: “Sasa kama ni kweli mbona ofisi yako bado ipo nyumbani kwa akina Ray? (Sinza-Mori).”
Johari: “Kazi zinakwenda kama kawaida. Mimi na Ray kwenye kazi hatuna tatizo lolote, asubuhi nafungua ofisi baadaye watu wanakwenda ‘lokesheni’.”
Ijumaa: “Hebu niambie kuhusu Mainda. Wakati unaingia kwenye uhusiano na Ray ulijua kuna Mainda?”
Johari: “Ndiyo nilijua.”

Ijumaa: “Ikawaje ukaingia sasa?”
Johari: “Hilo swali silitaki.”
Ijumaa: “Oke, je wewe na Mainda mna mawasiliano mazuri?”
Johari: “Yes! Ikibidi kuwasiliana tunawasiliana, tuko sawasawa.” 


Nguli wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ akiwa na mpenzi wake Chuchu Hans. Ijumaa: “Inasemekana umefunga pub yako ya kuuza pombe, ni kweli?”

Johari: “Ilibidi nifunge, mwenye nyumba alisema hapendi niuze pombe pale, natafuta sehemu nyingine.”
Ijumaa: “Nashukuru sana Johari.”
Johari: “Poapoa.”
GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...