2015-01-09

Mambo Hayo;Yanga Yatangaza Rasmi Kumtema Kipa Juma Kaseja


Uongozi wa Yanga rasmi umemtema kipa Juma Kaseja na kumtakia kila la kheri aendako.



Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kuachana na Golikipa wake Juma Kaseja kuanzia leo baada ya kuwepo kwa hali ya kutoelewana baina ya kipa huyo na uongozi wa klabu.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro amethibitisha taarifa hizo na kusema kuwa Juma Kaseja alivunja masharti ya mkataba huo kwa kutohudhuria mazoezini na kuongeza kuwa Jumamwenyewe alishaonesha nia ya kuondoka klabuni hapo hivyo ni bora klabu hiyo ikamuachia.

Muro amesema “Yanga haijavunja mkataba na Kaseja bali imemuachia baada ya Kaseja mwenyewe kuvunja masharti ya mkataba kati yake na Yanga...”
Kaseja alijiunga na Yanga baada ya kuwa huru kutokana na Simba kumuacha.


Kaseja ni kati ya makipa wakongwe nchini ambao wamewahi kung’ara akiwa Simba na timu ya taifa, Taifa Stars.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...