2015-01-28

Maskini;Maskini Wastara, Akiri Kushuka Kisanii Toka Mumewe Afariki Dunia



STAA wa filamu nchini, Wastara Juma amesema anajihisi kupoteza mwelekeo unaomfanya kushuka kisanaa tokea kufariki kwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kwani ari yake ya kufanya kazi imepotea.


Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, alisema Sajuki alikuwa ni msaada mkubwa sana kwake kisanaa mbali na maisha ya kawaida, kwani anashindwa kupita njia alizokuwa anapitishwa na mumewe huyo kiasi cha kujikuta akitoa filamu kati ya mbili hadi tatu kwa mwaka.

“Nikiri tu kwamba nimeshuka kisanaa, kasi ya kipindi kile imepungua, mume wangu alikuwa akijituma kuhakikisha mikakati yetu inaenda, kwa mwaka mzima nilitoa filamu hata tatu lakini toka asa naambulia moja tu mwaka mzima,” alisema.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...