Diamond Platnumz
Diamond Platnumz hana njaa na ndio maana alizikataa dola 30,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 54 za Tanzania kufanya show nchini Uganda?
Hiyo ni kwa mujibu wa rapper maarufu wa Uganda, Atlas Da African aliyekuwepo nchini wiki hii, baada ya Diamond kuwa chanzo cha kuijaza club Guvnor kwenye All White CIROC Party iliyoandaliwa na mpenzi wake Zari the Bosslady December 18 mwaka jana, makampuni kadhaa yalijitokeza kumtaka msanii huyo afanye show yake mwenyewe.
Kwa mujibu wa Atlas, kampuni moja ilimpa ofa hiyo Diamond ambaye hata hivyo alikataa.
Akiongea kwenye kipindi cha Clouds E cha Clouds TV, Atlas alidai kuwa hiyo ilionesha ni kiasi gani Diamond ana msimamo kwakuwa anajua kwa sasa kila mtu anamfahamu nchini humo na anaweza kupata fedha nyingi zaidi ya hizo.
Hata hivyo meneja wa Diamond, Salam amekanusha msanii wake kukataa kiasi hicho cha fedha.
“Hakuna show iliyokataliwa ila tulikuwa tunaongea na middle man sasa sijui yeye aliwaambia waandaji kiasi gani, plus walikuwa wanataka club appearance na show the next day kwa bei ya show peke yake kwahiyo show haikukataliwa tulikubaliana bei lakini hawakurudi tena,” Salam ameiambia Bongo5
0 comments:
Post a Comment