SAIDI Chigunda ni mmoja kati ya wasanii wakubwa wanaotingisha anga la Bongo Fleva hivi sasa.
Ingawa hayupo katika levo za kujidai sana, lakini ni kutokujua tu kunakoweza kukufanya umtoe katika kumi bora za wasanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini.
Amepiga kazi nyingi sana zinazomfanya kuwa juu tangu alipojiunga na Kundi la TMK Wanaume Family, wakati huo watoto wa Temeke wakiwa kitu kimoja chini ya uongozi wa Said Fella ‘Mkubwa’ ambaye licha ya kuwa hakamati kipaza sauti, lakini ametoa mchango mkubwa sana kwa mafanikio yanayosemwa kuwa nayo wasanii wanaounda kundi hilo.

Nimemfahamu Chegge kama msanii chipukizi wakati ule akiingia kwenye game na nimeshuhudia maendeleo yake hadi sasa ninapomtamka kama nyota.
Kilichonivuta kumzungumzia huyu jamaa, ambaye kule mitaa ya Sinza, jijini Dar es Salaam anafahamika kama mtoto wa Mama Saidi, ni kauli yake ya hivi karibuni aliyoitoa wakati akifanya mahojiano na waandishi wenzangu katika chumba cha habari cha Global Publishers.
Waandishi walikuwa wamemuuliza kama alikuwa na mpango wowote wa kufanya kolabo na mkali kutoka Temeke, Juma Kassim maarufu kama Nature. Katika majibu ambayo kwangu nayaona kama dharau, tena, ni pale aliposema kuwa Nature amekwisha, hawezi kufanya naye kolabo na wala hafikirii kabisa, kwa sababu akili yake iko zaidi katika namna ya ‘kutusua’ kimataifa!
Kwanza niseme wazi kwamba mimi siyo shabiki wa Nature, ingawa naheshimu sana uwezo wake katika muziki. Na siyo yeye tu, bali pia, sijawahi kuwa ‘mlevi’ wa ngoma za Chegge, japokuwa huwa natingisha kichwa ninaposikiliza kazi zake, hasa zile alizoshirikiana na Mheshimiwa Temba, kwa sababu huyu mchizi (Temba) huwa namfagilia kwa namna anavyonesanesa kwenye verse za kazi zake.
Ukweli usiopingika ni kwamba Nature alitangulia katika fani na hata umaarufu pia, miaka kadhaa kabla Chegge hajaja na kuwa chini ya uongozi wake (TMK Wanaume Family).

Hatuwezi kubishana hapa kujadili suala hili kwa sababu liko wazi, ndiyo maana kwa nguvu na uwezo aliokuwa nao, alikuwa na ujasiri wa kuamua kujing’oa katika kundi, pale alipohisi ‘kuzinguliwa’ na Fella, ujasiri ambao Chegge hakuwahi kuwaza kuwa nao!
Kwamba Nature amekwisha, siwezi kupinga wala kukubali, kwa sababu kidogo miaka ya karibuni nimekuwa mbali nao kikazi. Iwe ni kweli amekwisha makali, au iwe si kweli, tatizo langu halipo huko, ninachojadili mimi ni heshima, ambayo kimsingi nadhani inatakiwa kuwepo baina ya wasanii hawa.
Inawezekana kabisa kuwa kiwango cha sasa cha Nature hakiwezi kumvutia Chegge kupiga naye kazi, kwa sababu hawezi kumsaidia katika ndoto zake za kuelekea kutambulika kimataifa, lakini busara za kawaida zinatushawishi tuamini kuwa ni ukosefu wa heshima kwa maneno kama hayo kutamkwa kuhusu mkongwe huyu mwenye mchango usiopingika katika Bongo Fleva.

Wasanii wetu wanakosa busara za kujua nini cha kusema na kwa wakati gani. Swali hilo, ili kuonyesha weledi alionao, angeweza kulijibu kirahisi tu; “Kwa sasa sina project yoyote ya kumshirikisha Nature, lakini nikipata ningependa kufanya naye kazi!” Simple!
Lakini kauli ile, ya kwamba Nature amekwisha, lengo lake ni kumtangaza Kibla kuwa enzi zake zimekwisha na hana tena thamani. Chegge anasahau kuwa Nature ana mashabiki wengi kuliko yeye na kauli hiyo inaweza kumpunguzia watu wa kumuunga mkono.
Lakini labda kitu tunachoweza kujifunza ni kutambua kuwa unaweza kudharau kitu au mtu, lakini busara inatuongoza kutopaza sauti kusema hisia zetu katika eneo ambalo tungeweza kujidhibiti.
Kimuziki Nature ni mkubwa sana kwa Chegge, hata kama anamzidi ubora kwa kazi za sasa, kitu ambacho hakimpi haki ya kumletea dharau!
GPL.
0 comments:
Post a Comment