BAADA ya kukulia katika maisha ya kimasikini kwa kipindi kirefu, Mwalimu Bora wa Ujasiriamali nchini Tanzania, Eric James Shigongo anatarajia kuanza semina ya ujasiriamali iitwayo KUTOKA UFUKARA MPAKA UBILIONEA, itakayofanyika Tandale jijini Dar es Salaam.
Eric James Shigongo.
Lengo kubwa la kufanya semina hiyo ni kumkomboa kijana masikini aishiye Tandale ahame kwenda sehemu ya watu wanajiona kuwa matajiri, Masaki au Oysterbay na kwingineko, yote inawezekana.
Diamond Platnumz.
Somo kubwa atakalofundisha ni Jinsi ya Kuhama Kutoka Kwenye Umasikini Kwenda Kwenye Mafanikio. Katika semina hiyo, hatokuwa peke yake bali kutakuwepo na walimu wengine maarufu Tanzania kama James Mwang’amba na Dk. Didas Lunyungu, pia ili kuwaonyeshea vijana kwamba inawezekana, msanii mwenye jina kubwa, aliyetokea uswahilini, Diamond Platnumz atakuwepo kwa ajili ya kuzungumza na vijana.
James Mwang’amba.
Semina hiyo itaanza tarehe 2/4/2015 mpaka 4/4/2015 katika Uwanja wa Gengeni (Kwa Sharifu) hapo Tandale Mbuyuni na hakutokuwa na kiingilio chochote kama ilivyo sehemu nyingine, elimu yote hiyo itatolewa BUREEEEE.
Karibuni sana.
Dk. Didas Lunyungu.

0 comments:
Post a Comment