NYUMBA zaidi ya 200 zimezingirwa na maji baada ya mvua kubwa kunyesha hali iliyosababisha mafuriko makubwa na kuzua taharuki kwa wakazi wa maeneo ya Kiyangu B, Kisutu, Ligula na Mdenga.
Mvua hiyo iliyoanza kunyesha saa 8 usiku wa kuamkia jana hadi saa 11 alfajiri imeharibu makazi ya watu na miundombinu katika mji wa Mtwara.
Kutokana na hali hiyo iliulazimu uongozi wa mkoa kuitisha kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ambapo walijadili hali hiyo na kufanya ziara ya kukagua maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea maeneo yaliyoathirika, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu, alitoa saa 24 kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kutafuta ufumbuzi wa kuyaondoa maji yaliyojaa katika makazi ya watu ili kuweza kunusuru uhai wa wananchi.
“Maji ni mengi yamezunguka makazi ya watu, hali hii inatisha sana na katu hatuwezi kukaa huku Watanzania wenzetu wakiendelea kupata adha kutokana na maji ya mvua yaliyojaa katika makazi yao.
“Hatua za haraka zichukuliwe kudhibiti hali hii, mganga mkuu wa mkoa achukue hatua za haraka za kupiga dawa ili kuweza kuwakinga wananchi na magonjwa ya milipuko ila ninawaomba wazazi kuwa makini na watoto, hasa katika kipindi hiki cha mafuriko,” alisema Dendegu.
Akizungumza na MTANZANIA, Alia Chilema, mkazi wa Kisutu (Nabwada), alisema Serikali imekuwa na tabia ya kuwatembelea tu bila kutoa suluhu ya tatizo la maji kujaa na kuathiri nyumba zao hali inayowafanya waishi kwa shaka.
Alisema bwawa la Nabwada limekuwa ni mradi wa viongozi jambo linalosababisha wananchi kutosikilizwa kilio chao cha muda mrefu hali ambayo inawasababishia kupoteza mali nyingi ikiwamo pesa Sh 300,000 alizopoteza baada ya maji kuingia ndani.
“Mimi najua Serikali ina uwezo wa kuhamisha maji haya na kuweka mifereji yakaelekea baharini, sio mbali kutoka hapa, lakini kwakuwa huu ni mradi sisi wanyonge tunaumia sana, viwanja hivi vimepimwa na hati tunazo, kwanini hatusaidiwi na Serikali yetu kila mwaka tunapata hii shida?” alisema Chimwela.
Naye Tatu Mkaugala mkazi wa Kiangu B, alisema kitendo cha maji kujaa na kuzingira makazi yake amepata hofu na kuhitaji msaada ili aweze kuishi kwa amani na familia yak
0 comments:
Post a Comment