Dar es Salaam. Kuna njia mmoja tu ya kupambana na vijana waliokata tamaa ya maisha maarufu kama Panya Road waliopo katika jiji la Dar es Salaam.
Ni rahisi kuwadharau vijana hao, lakini makundi yote makubwa ya kigaidi au yale ambayo yanasumbua nchi mbalimbali duniani yalianza kimasihara hivihivi kama walivyo Panya Road wa Dar es Salaam.
Hawa ni vijana ambao wamekataa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini. Wamefika katika hatua ya ‘alienation’ au kwa lugha nyepesi unaweza kusema wamejikataa au kudhani dunia imewakataa.
Ni rahisi kuwadharau vijana hao, lakini makundi yote makubwa ya kigaidi au yale ambayo yanasumbua nchi mbalimbali duniani yalianza kimasihara hivihivi kama walivyo Panya Road wa Dar es Salaam.
Hawa ni vijana ambao wamekataa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini. Wamefika katika hatua ya ‘alienation’ au kwa lugha nyepesi unaweza kusema wamejikataa au kudhani dunia imewakataa.
Kisaikolojia, ‘alienation’ ni hatua ya mwisho kabisa kabla ya mtu kuamua kujiua. Ndiyo maana watu wanaodhani vijana hawa ni wahuni wanakosea, badala yake wanapaswa kujua sababu kuu inayowafanya wafanye vurugu na si kuwalaumu tu.
Vijana hawa wamejikataa na ndiyo maana hawataki kujiita majina ya binadamu, badala yake wamejipachika majina ya wanyama kama ‘panya’ au watoto wa mbwa mwitu. Kwa hatua waliyofika, huwezi kuwadharau tena kama viongozi wetu wanavyofanya sasa kwa kutoa lugha ya vitisho.
Ni rahisi kwa Serikali kusema ‘tutawadhibiti’, lakini kuna njia moja kubwa ya kuwadhibiti ambayo itakuwa ni suluhisho la kudumu na si kutumia nguvu kama dola inavyofanya.
Hawa vijana wamekata tamaa ya maisha, hawana kazi, wamekuwa wakiishi kwa mfumo wa uchumi unaoitwa ‘hand to mouth’ yaani ‘mkono kwa mdomo’, kila wanachokipata kwa siku kinakwenda mdomoni, hawana akiba yoyote.
Hawawezi kuweka akiba yoyote, kila wanachokipata wanakitumia leo na hawana uhakika wa kesho. Hayo ndiyo maisha yao ya kila siku. Kwao hakuna maisha bora kwa kila Mtanzania ila kuna bora maisha kwa kila Mtanzania.
Inapofikia hali hiyo, binadamu huwa anakataa tamaa na inapofika hatua hiyo mtu huwa hajui sababu inayomtia hasira na ndiyo maana ukiwauliza vijana hao wa Panya Road kwa nini wanapora mali za watu watakwambia kwa sababu mwenzao kauawa, kapigwa au kakamatwa na polisi. Huwa hawajui sababu ya msingi kwa kuwa imejificha.
Wanachokieleza huwa si sababu ya msingi, bali kichocheo tu cha sababu ya wao kuibuka barabarani na kupora mali za watu na kuwaacha wengi wakiwa na maumivu kutokana na vipigo.
Sababu kubwa za kuibuka makundi kama haya ni kwamba rasilimali nyingi za nchi zimeshikiliwa na watu wachache na kwamba hakuna mgawanyo sawa wa rasilimali hizo kwa watu wote. Kuna wachache wanachukua kila kitu wakati wapo wengi ambao hawapati kabisa.
Unapoambiwa nchi hii ina madini, ina mbuga za wanyama, bahari, Mlima Kilimanjaro, mito, maziwa, misitu na rasilimali nyinginezo unashangaa kuona kuna kundi kubwa la watu wakiishi maisha ambayo hayana uhakika wa kesho.
0 comments:
Post a Comment