2015-01-16

Hayo ndiyo maneno ya Mwigizaji Mlela Atangaza Kuoa Mwaka Huu kwani amechoka kukaa ukapela


MSANII wa filamu za Kibongo, Yusuf Mlela amefunguka kwamba baada ya kuishi ‘singo’ kwa muda mrefu, sasa anajipanga kuoa hivyo ndani ya mwaka huu lazima ndoto yake hiyo itimie.

Akipiga stori na gazeti hili, Mlela alisema mwaka huu amejiwekea malengo mengi lakini kubwa zaidi ni kuoa kwani anahisi akiendelea kuwa peke yake kuna mambo atakwama kwa kuwa hatakuwa na mtu wa kumshauri kwa karibu.

“Kiukweli maisha yenyewe ni mafupi na umri nao unaenda hivyo lengo langu kubwa kwa mwaka huu ni kuoa na kuhusu nitamuoa nani itajulikana baadaye lakini kwa sasa tambueni kwamba mwaka huu lazima nioe, nimechoka maisha ya ubachela,” alisema Mlela ambaye ameingia kwenye Top 3 ya Ijumaa Sexiest Bachelor kwa mwaka 2014-15. 
 

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...