Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali ya basi la Kampuni ya Saratoga linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Dar es Salaam, iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kaguruka Kijiji cha Bweru Kata ya Itebula Wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma, wakati basi hilo likitoka Dar es Salaam kwenda Kigoma.
Mganga wa zamu katika Kituo cha Afya cha Nguruka, Dr.Beatrice Mtesigwa, amemtaja aliyefariki katika ajali hiyo kuwa ni Adam Kaimbe mwenye umri wa miaka 28, mkazi wa Mwanga mjini Kigoma, ambaye ni kondakta wa basi hilo, ambaye amefariki muda mfupi baada ya kufikishwa katika kituo cha afya cha Nguruka kwa ajili ya matibabu.
Amesema kuwa marehemu amefariki dunia baada ya kuvuja damu nyingi kupitia sehemu za puani na masikioni kutokana na kuumia sana kichwani.
“Marehemu aliumia sana sehemu ya kichwani; tumejitahidi sana kuokoa maisha yake kadiri ya uwezo wa kituo chetu lakini imeshindikana sababu kichwa chake kilikuwa kimebonyea na alivuja damu nyingi sana,”alisema Dr.Mtesigwa.
“Marehemu aliumia sana sehemu ya kichwani; tumejitahidi sana kuokoa maisha yake kadiri ya uwezo wa kituo chetu lakini imeshindikana sababu kichwa chake kilikuwa kimebonyea na alivuja damu nyingi sana,”alisema Dr.Mtesigwa.
Said Goro ni mmoja wa majeruhi Wawili akiwa Hospitalini
Aidha amewataja majeruhi wa ajali hiyo ni Said Goro mwenye umri wa miaka 32, mkazi wa Kigoma, ambaye amevunjika miguu yote miwili na mkono wa kulia na dereva wa basi hilo Ramadhani Mohamed mwenye umri wa miaka 47, ambaye amepata maumivu sehemu ya mgongo wake.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment