Watuhumiwa wakisubiri kupewa dhamana katika chumba cha kusikiliza kesi.Wafuasi wa CUF wakishuka kwenye ngazi kutoka katika chumba cha kusikiliza kesi baada ya kupewa dhamana. Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Taifa wa CUF, Abdallah Kambaya (katikati) akitoka lango kuu la Mahakama baada ya kupewa dhamana akishikwa mkono na mfuasi wa chama hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Magdalena Sakaya (kushoto) akiwa na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Taifa, Abdallah Kambaya (kulia).
WAFUASI 29 kati ya 30 wa CUF waliokamatwa kwenye jaribio la maandamano ya kuwakumbuka wafuasi wenzao waliouawa mwaka 2001, Mbagala-Zakhem jijini Dar sanjari na mwenyekiti wao, Prof. Ibrahim Lipumba, mchana huu wameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wafuasi hao wameachiwa leo kwa dhamana baada mwenyekiti wao kupandishwa kizimbani juzi katika Mahakama Kisutu kujibu kesi ya kuhamisisha wafuasi wa chama hicho kutenda kosa la jinai kuhamasisha maandamano Januari 27, mwaka huu.
Wafuasi hao 29 walikidhi vigezo vya udhamini na kuachiwa lakini mwenzao mmoja ambaye aliendelea kushikiliwa hadi pale baada ya mdhamini wake kuchelewa kutimiza masharti ya dhamana.
Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru alisema shauri hilo litasikikilizwa tena Februari 12, mwaka huu.
gpl
0 comments:
Post a Comment