Maskini! Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ yu mgonjwa tena, safari hii ameibuka na kueleza maradhi ambayo yanamsumbua akisema: ‘Ugonjwa huu utaniua.”
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’.
Awali Ijumaa Wikienda lilipokea taarifa juu ya kuumwa kwa Banza ambapo ilielezwa kuwa, alilazimika kusafirishwa kutoka Mbeya hadi Dar baada ya hali yake kiafya kuwa mbaya.
AJIKONGOJA
Hivi karibuni, gazeti hili lilimfuata nyumbani kwake Sinza ya Vatican jijini Dar na baadaye alijikongoja na kwenda kwenye Ukumbi wa Flamingo uliopo Magomeni ndipo akazungumzia kinachomtesa.
KICHWA
Banza ambaye siku hizi hupenda kujiita Roho ya Paka alisema kuwa kinachomsumbua ni maumivu ya kichwa hasa wakati wa jua kali.
KIZUNGUZUNGU
“Kichwa kinaniuma sana hasa wakati wa jua kali, mishipa ya kichwa inaniuma sana halafu nasikia kizunguzungu muda wote, sifahamu ni kwa nini,” alisema mwanamuziki huyo akionekana kuwa na maumivu makali.
‘Banza Stone’ akiuguza ugonjwa.
Jamaa huyo alisema kuwa anaendelea na tiba akisaidiwa na mama yake, Hadija.
Jamaa huyo alisema kuwa anaendelea na tiba akisaidiwa na mama yake, Hadija.
“Kwa sasa nipo tu nyumbani, natazama afya yangu, ukweli nahitaji matibabu ya nguvu ili kunirejesha kwenye hali yangu ya kawaida,” alisema Banza.
MSAADA WA MADAKTARI
Hata hivyo, Banza alisema hataki kuomba msaada wa kuchangiwa fedha ili kupata matibabu ila anachoomba ni madaktari ambao wanafahamu tiba ya ugonjwa huo ili wamsaidie kimatibabu.
Si mara ya kwanza kwa Banza kuumwa kwani mara kadhaa alisharipotiwa kuwa hoi kwa magonjwa mbalimbali ikiwemo kifua.
KUTOKA KWA MHARIRI
Ijumaa Wikienda linamtakia Banza afya njema ili arejee jukwaani kuwapa burudani mashabiki wake na madaktari wanaoona wanaweza kumtibu, wajitokeze.
GPL
0 comments:
Post a Comment