Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amekoleza moto wa sakata la mabilioni ya fedha zinazodaiwa kufichwa benki nchini Uswisi kwa kuzitaka mamlaka zinazochunguza, kuzitaifisha ili zitumike kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.
Nchemba alitoa wito huo jana wakati akizungumza katika mahojiano na kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Kituo cha Redio One nchini.
“Kuficha fedha nje ni uhujumu uchumi kwani fedha yeyote iliyofichwa nje ni lazima itakuwa imepatikana kwa njia zisizokuwa halali na mtu wa namna hiyo anatakiwa fedha zake zitaifishwe zisaidie katika maendeleo na kusomesha yatima,”alisema.
Alisema takwimu zinaoonyesha kuwa fedha zinazoombwa katika mataifa yaliyoendelea duniani zinazotoroshwa na kufichwa nje kutokana na rushwa au matumizi mabaya ya madaraka hali inayodidimiza maendeleo ya nchi.
0 comments:
Post a Comment