Lupita Nyong’o alikuwa mmoja ya wanamitindo na mastaa ambao walipendezesha Red Carpet na event yote ya sherehe za Tuzo za Oscars mwaka huu ambazo zilifanyika siku ya Jumapili February 22 Marekani.
Kuanzia siku ya jana kuna story ambayo ime hit vichwa vya habari vingi kuhusu Lupita, lile gauni lake kali ambalo alivaa siku ya event hiyo limeibiwa katika chumba cha Hotel ambayo alikuwemo staa huyo.
Thamani ya gauni ni dola 150,000/-, sio hela ndogo kiukweli, ni kama mil. 270 Tshs.
Gauni hilo lilikuwa maalum kwa ajili ya Lupita, lilitengenezwa na Calvin Clain.
Hotel hiyo ya London Hotel iliyopo Hollywood wamesema kuwa wanashirikiana na Polisi kufanya upelelezi kukagua picha za kwenye camera ya CCTV, wanaamini aliyeiba atapatikana kwa kuwa kama mtu alitoka amelibeba lazima wataweza kumgundua kutokana na ukubwa na uzito wa gauni hilo.
Chumba cha Lupita kilikuwa busy kutokana na watu wengi kuingia humo ikiwemo watu wa mitindo, make up, mameneja na marafiki zake wa karibu pia.
0 comments:
Post a Comment