Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP) ametoa shutuma zake bungeni Dodoma akimtuhumu mbunge James Mbatia kuwa amekuwa akimpakazia mambo mabaya kwa wapiga kura wa jimbo lake kuwa ana UKIMWI.
Mrema amesema kuwa mbunge huyo amekuwa akipita jimboni kwake na kusema kuwa wasimchague mbunge huyo kwa kuwa ana UKIMWI na hana maisha marefu hapa duniani.
Ametoa kauli hiyo bungeni Dodoma na kusema "Napenda kusema kuwa mimi ni mbunge halali wa Vunjo na Mbatia hatapata jimbo hilo, na natangaza kuwa nitagombea tena na hafi mtu hapa"
0 comments:
Post a Comment