2015-02-21

ODAMA AFUNGUKA KUCHANGIA WANAUME! MAMBO YAKO HAPA JIONEE NISHIDAAAAAAAAAAA


MAMBO yanazidi kunoga ndani ya safu hii ya Sindano 5 za moto, kutokana na maombi yenu, leo tumemleta kwenu mwigizaji Jeniffer Kyaka ‘Odama’, tiririka naye:

Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Jeniffer Kyaka ‘Odama’.

Paparazi: Mambo vipi Odama! Tuanze moja kwa moja na swali la kwanza, hivi kwa sasa una mpenzi? Mbona hatumjui?Odama: Mambo poa! Mpenzi ninaye, nampenda muda bado wa kumuanika.Paparazi: Ulishawahi kuchangia bwana na mwanamke mwingine katika maisha yako?
Odama: Hapana, sina kumbukumbu hiyo.

Paparazi: Hadi leo hii unaweza kukumbuka idadi ya wanaume ambao umewahi kutoka nao kimapenzi?
Odama: Nakumbuka, kama mtu hukumbuki idadi basi lazima utakuwa una kichaa. Nakumbuka kwa sababu idadi ni ndogo, ila hapa sitataja idadi yao. Paparazi: Hivi baba mtoto wako ni nani hasa au ndiye uliyenaye hadi sasa?
Odama: Hilo liweke kapuni kwa sasa, nitalizungumza ‘next time’.Paparazi: Inasemekana wewe ni miongoni mwa warembo ambao wanaoongoza kwa kutongozwa Bongo Movies, ni kweli?
Odama: Hiyo kawaida kwa mtoto wa kike, nadhani sipo peke yangu.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...