2015-02-09

Mbasha: Simtambui mtoto wa Flora.............hebu soma alichokisema


Baada ya mchungaji maarufu nchini, Gwajima kukanusha kuwa si baba wa mtoto wa Flora Mbasha, mume wa muimbaji huyo wa muziki wa injili, Emmanuel naye amesema hatambui chochote kuhusu kuzaliwa kwa mtoto huyo. 


Mbasha ambaye pia ni muimbaji wa muziki huo amesema ana mtoto mmoja mwenye umri wa miaka kumi na kwamba taarifa za kuwa Flora amejifungua anazisikia kama watu wengine. 


“Nina mtoto mmoja, nina mtoto mmoja anaitwa Lizy na ana kama miaka 10 hivi. Wewe ndo unanieleza mimi kama amejifungua, kama amejifungua ni jambo jema na jambo la kumshukuru Mungu,” Mbasha alikiambia kipindi cha Sunrice cha Times FM.


0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...