Mrema alisema wanaowania jimbo lake wamefilisika kisiasa na kutumia ugonjwa wake kama njia ya kuwania jimbo hilo
Dar es Salaam. Wakati Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema akiahidi kuwasilisha taarifa ya ugonjwa unaomsumbua bungeni leo ili kuwanyamazisha wanaochafua, Kada wa CCM, Profesa Mwedadi Mbaga ametangaza kuwania kiti cha jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Mrema alisema amechoka kudhalilishwa na watu wanaotaka kuwania ubunge Jimbo la Vunjo.
Dar es Salaam. Wakati Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema akiahidi kuwasilisha taarifa ya ugonjwa unaomsumbua bungeni leo ili kuwanyamazisha wanaochafua, Kada wa CCM, Profesa Mwedadi Mbaga ametangaza kuwania kiti cha jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Mrema alisema amechoka kudhalilishwa na watu wanaotaka kuwania ubunge Jimbo la Vunjo.
“Mimi ni mzima, nina nguvu na nitagombea ubunge kwenye jimbo langu kwa garama yoyote,” alisema Mrema na kuongeza:
“Nataka kuwasilisha taarifa bungeni kutoka kwa madaktari wangu, itaeleza kinachonisumbua.”
Alisema taarifa atakoyowasilisha bungeni ni kipimo cha TC scan kutoka kwa madaktari wa Hospitali ya Apollo ya India pamoja na taarifa iliyotolewa na daktari wake kuhusiana na mabakabaka yalipo usoni mwake.
Alisema dhumuni la kuwasilisha taarifa hizo ni ili wananchi wasikie ukweli na siyo uongo kama unavyoenezwa.
Wakati huohuo, Profesa Mbaga amesema atagombea nafasi ya ubunge Jimbo la Vunjo katika uchaguzi ujao.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka Falme Kiarabu anakofanya kazi, Profesa Mbaga alisema amefikia hatua hiyo baada ya kuombwa na wazee wa jimbo hilo pamoja na utashi wake kutaka kuwatumikia wananchi wa Vunjo.
“Mimi ni mtoto wa mkulima, ni kada wa CCM tangu nasoma Sekondari. Nitagombea ubunge katika uchaguzi ujao kupitia CCM,” alisema Mbaga ambaye ni mhadhiri Chuo Kikuu cha Sultan Qaboos, Oman.
Profesa Mbaga aliyewahi kufanya kazi serikalini, anaungana na Innocent Melleck (32) pia wa CCM aliyetangaza kuwania jimbo hilo pamoja na mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi kati ya mwaka 1995 hadi mwaka 2000.
Awali, hatua ya Mbatia kutangaza nia hiyo ilimwingiza katika malumbano na Mrema, ambaye pia alimshtaki kwa Rais Jakaya Kikwete akitumia vikao kati ya viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Rais vilivyofanyika Dodoma mwaka jana kufikisha malalamiko yake hayo.
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment