2015-02-05

Polisi auawa akiokoa mtoto asiuawe na baba yake mzazi inahuzunisha sana.................bofya hapa kuona mauaji


Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Misime.
Askari Polisi PC Joseph Swai, ameuawa wakati akimwokoa mtoto wa miezi minane, aliyekuwa akiteswa na baba yake mzazi katika mtaa wa Chang'ombe Juu mjini hapa.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Misime, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 5:00 asubuhi na kumtaja mtoto aliyekuwa anateswa kuwa ni Valerian Mallya.


Alisema awali, polisi huyo alipigiwa simu na Mtendaji wa mtaa wa Chang'ombe Juu, akimjulisha kuwa amepokea taarifa kutoka kwa Oliva Baltazar (52), kuwa kijana wake, Tisi Mallya (29), anamtesa mtoto wake.

Alisema polisi huyo alikwenda eneo la tukio na alipofika aligonga mlango huku akijitambulisha kuwa ni askari, kisha akamuamuru atoke nje.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...