2015-02-05

Boko Haram wafanya mauaji Cameroon cheki video ya mauaji hapa..............




Wanamgambo wa Boko Haram wamewaua zaidi ya watu 100 katika mji wa Fotokol ulioko kaskazini mwa Cameroon. 
Viongozi wa kikabila wamesema watu hao wameuawa baada ya Boko Haram kuwavamia katika nyumba zao, mitaani na kwenye msikiti. Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Cameroon idadi kamili ya watu waliouawa bado haijulikani. 
Mauaji hayo yamefanyika muda mfupi baada ya majeshi ya Chad kuwaua zaidi ya wapiganaji 200 wa Boko Haram, wakati waasi hao walipoishambulia kambi yao ya kijeshi iliyoko Cameroon. 

Nigeria, Cameroon na Chad zimeongeza mapambano makali dhidi ya waasi wa Boko Haram ambao wamekuwa wakiwateka nyara na kuwaua watu nchini Nigeria kwa lengo la kutaka kuanzisha taifa la kiislamu.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...