2015-02-03

Sad News: Dereva wa OCD wilaya ya Manyoni ajipiga risasi na kufariki





DEREVA wa OCD wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida,Aloyce Alibinus amefariki dunia papo hapo baada ya kujipiga risasi mdomoni na kutokea kisogoni.

Akizungumza kwa njia ya simu, OCD wilaya ya Manyoni ASSP, Alute Yusufu Makita,amesema tukio hilo limetokea jana februari mbili saa tano asubuhi Manyoni mjini.

Akifafanua alisema kuwa asubuhi ya jana dereva wake bila yeye kujua alikwenda kwenye ghala la kutunzia silaha na kuomba bunduki kwa madai kuwa wanaenda na bosi wake vijijini kikazi. 



Alisema kuwa baada ya Alyoce kufanikiwa kupewa bunduki hiyo,aliondoka moja kwa moja akarejea nyumbani kwake na kufungulia radio kwa sauti kubwa.

“Baada ya hapo Alyoce alipanua mdomo na kisha kujipiga risasi moja kinywani na ilitokea kisogoni na kuunguza mto wa kitanda na kisha ukuta.Majirani hawakuweza kusikia mlio wa risasi kutokana na sauti kubwa ya radio.

Alisema dereva huyo hajaacha ujumbe wo wote juu ya uamuzi wake huo wa kujikatisha maisha na kudai kwamba taarifa zaidi itatolewa na kamanda wa jeshi la polisi baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa tukio hilo.

Katika tukio jingine,habari za uhakika kutoka New Kiomboi wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,zinadai afisa elimu sekondari leo asubuhi alizirai baada ya kuzuka kwa malumbano makali kati yake na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Halima Mpita.Inadaiwa malumbano hayo yalihusu bomu lililowekwa kwenye bahasha lililolengwa kuuawa mkurugenzi huyo. 


Akizungumzia tukio hilo, mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda, amekiri kwamba ni kweli afisa huyo alikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Iramba na kwamba sababu ya kufikishwa hospitali bado hazijajulikana. Nawanda amedai kuwa afisa huyo elimu sekondari, ameahidi akitoa hospitali, atampa taarifa ya mkasa huo.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...