2015-02-03

AIRTEL NOUMAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!! INAWALETEA WATEJA WA AIRTEL KUSHINDA GARI MOJA KILA SIKU‏

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Levi Nyakundi (kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Beatrice Singano Mallya (kulia) wakionyesha kipeperushi wakati wakizindua rasmi promosheni ya 'Airtel Yatosha Zaidi' ambapo wateja watakaojiunga na bando la yatosha watapata nafasi ya kushinda kila siku gari moja aina ya Toyota IST. Uzinduzi wa promosheni hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Levi Nyakundi (kulia) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Beatrice Singano Mallya (kushoto) wakionyesha baadhi magari yatakayoshindaniwa wakizindua rasmi promosheni ya 'Airtel Yatosha Zaidi' ambapo wateja watakaojiunga na bando la yatosha watapata nafasi ya kujishindia kila siku gari moja aina ya Toyota IST. Uzinduzi wa promosheni hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.

Mwendesha baiskeli akifanya manjonjo yake wakati wa uzinduzi wa promosheni ya 'Airtel Yatosha Zaidi' ambapo wateja watakaojiunga na bando la yatosha watapata nafasi ya kujishindia kila siku gari moja
aina ya Toyota IST. Uzinduzi wa promosheni hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.

Mwendesha pikipiki akinyesha umahiri wake kunogesha wa uzinduzi wa promosheni ya 'Airtel Yatosha Zaidi' ambapo wateja watakaojiunga na bando la yatosha watapata nafasi ya kujishindia kila siku gari moja aina ya Toyota IST. Uzinduzi wa promosheni hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya AirtelTanzania, Levi Nyakundi (kushoto) akiwa na Balozi wa Promosheni yas Airtel Yatosha Zaidi, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ney wa Mitego katika hafla ya uzinduzi rasmi wa promosheni ya 'Airtel Yatosha Zaidi' ambapo wateja watakaojiunga na bando la yatosha watapata nafasi ya kujishindia kila siku gari moja aina ya Toyota IST. Uzinduzi wa promosheni hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.

Wateja wa Airtel kushinda gari Moja Kila Siku

· Kupitia huduma ya Airtel Yatosha

· Promosheni ya Airtel yatosha zaidi itawawezesha wateja wa Airtel kushinda Toyota IST moja Kila siku


Airtel Tanzania leo imezindua promosheni kabambe ijulikanayo kama Airtel Yatosha Zaidi kwa wateja wanaotumia vifurushi vya Airtel Yatosha kuweza kujishindia gari Aina ya Toyota IST kila siku

Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Masoko ya Airtel Bwana Levi Nyakundi alisema” promosheni hii ni nafasi ya peeke wa wateja wetu wanaojiunga na vifurshi vya Airtel yatosha vya siku, wiki na mwezi kupata faida zaidi kutokana pesa wanazozitumia. Nia yetu kuhakikisha tunatoa huduma na bidhaa bora kwa kupitia huduma yetu ya Airtel Yatosha huku tukiwazawadia wateja wetu zawadi nono.

Tunaamini promosheni hii itawapatia wateja wetu uzoefu tofauti wakati wote wakitumia huduma zetu za Airtel Yatosha. Zaidi ya wateja wetu kijishindia magari promosheni hii ya Airtel Yatosha Zaidi itawapatia wateja wetu vifurushi zaidi “Aliongeza Nyakundi Akiongea kuhusu namna ya kushiriki Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema” ili kushiriki kwenye promosheni hii wateja wanatakiwa kuendelea kununua vifurushi vyao vya Yatosha vya siku, wiki na mwenzi. hakuna gharama ya ziada, kwa kununua vifurushi vya yatosha tayari utakuwa umeunganishwa kwenye droo ya yatosha zaidi na kupata nafasi ya kujishinidia Toyota IST moja kila siku

Hii ni promosheni ya aina yake ambapo wateja wetu wanazawadiwa kutokana na matumizi yao ya kawaida ya vifurushi vya Yatosha. tunatoa wito kwa wale ambao hawajajiunga na vifurushi vya Airtel yatosha kufanya hivi na kupata nafasi ya kushinda gari moja kila siku”aliongeza Mallya

Kununua vifurushi vya yatosha wateja wanaweza au kupiga *149*99#, kunua kwa kupitia huduma ya Airtel Money au kwa kununua vocha ya Airtel yatosha inayopatikana katika maduka yetu nchi nzima

Mwaka Jana Airtel ilizindua huduma ya kisasa ya kibunifu na yenye vifurushi vya gharama nafuu sokoni. Kuzinduliwa kwa promosheni hii ya Airtel yatosha Zaidi ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel ya kutoa huduma bora huku ikiwazawadia wateja wake kwa kutumia huduma zake

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...