2015-02-20

WALIOZAA NA NAY ------------ BIFU LAO JIONEE MWENYEWE KILICHO SABABISHA



Mabinti wawili waliozaa na msanii wa muziki, Emmanuel Elbarik ‘Nay wa Mitego’, Siwema na Skyna Ally ambao awali ilidaiwa walikuwa na bifu zito, sasa wameamua kuwa mashosti.Ijumaa hivi karibuni liliwanasa wawili hao kwenye Ukumbi wa Escape One, Msasani jijini Dar wakiwa beneti kama mtu na mke mwenza na lilipotaka kuzungumza nao wote walichenga na kutaka waachwe.

Mrembo aliyezaa na msanii wa muziki, Emmanuel Elbarik ‘Nay wa Mitego’ Siwema.

Hata hivyo, mmoja wa marafiki aliyekuwa ameongozana nao aliyeomba hifadhi ya jina lake alimwambia mwandishi wetu kuwa, baada ya wawili hao kuwa na bifu kwa muda mrefu, waliamua kukaa chini na kumaliza tofauti zao kwani kilichotokea tayari kimeshatokea.

Skyna Ally. “Sasa hivi ni mashosti ile mbaya, sehemu mbalimbali wamekuwa wakienda pamoja, yaani ni kama vile wamekubali kuwa wake wenza licha ya kwamba anayekaa na Nay ni Siwema,” kilieleza chanzo hicho.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...