Akielezea kuhusu picha zilizosambaa kwenye mitandano ya kijamii, Ommy Dimpoz, alisema walikuwa Afrika Kusini kwa mapumziko ndipo picha hizo zilipopigwa.
“Tunapiga picha nyingi sana na Wema, hii siyo mara ya kwanza, lakini sijui kwanini hizi zimetengeneza taswira nyingine kwa mashabiki,” alisema.
Picha za wawili hao wakiwa katika pozi tofauti zimeendelea kuwa gumzo na kuzua maswali mengi kwa mashabiki, kutokana na ukaribu aliyonao Ommy Dimpoz na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Wema, Nasib abdul ‘Diamond’.
0 comments:
Post a Comment