MSANII wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amefunguka kuwa anaamini amepigwa ‘juju’ kutokana na kuugua ugonjwa ambao haukutambulika hospitalini.
“Roho inaniuma sana yaani ni jinsi gani wasanii tulivyokuwa hatupendani, ghafla tu nilipofika nyumbani baada ya kutokea Moro kwenye dili la kazi hali yangu ilibadilika, nikahisi kichwa kuniuma sana na maumivu makali tumboni, nilipoenda hospitali niliambiwa sina tatizo ikanilazimu nitafute mtaalamu na kuyabaini hayo maana lengo lao walitaka kunimaliza, nashukuru Mungu kwa sasa nimepata nafuu,” alisema Bozi.
0 comments:
Post a Comment