2015-03-05

INTERVIEW YAKAJALA KUHUSU MAISHA YAKE YA JELA............bofya hapa kuisoma


 Paula (kushoto) akiwa na mama mlezi pamoja na mdogo wake.
MAMBO vipi mpenzi msomaji wa safu hii? Kama kawaida ni hapa tunakutana na mastaa waliobarikiwa kupata watoto na kuzungumza nao kuhusu maisha yao ya kila siku.
 Leo tunaye mwanadada ambaye miezi michache iliyopita alikumbana na misukosuko ya kutupwa nyuma ya nondo kisha kuachiwa kwa kulipa faini, Kajala Masanja. 

Kajala ana mtoto mmoja aitwaye Paula (11) ambaye alizaa na prodyuza mkongwe Bongo, Paul Mathyasse ‘P Funk.
Ungana nami katika mahojiano niliyofanya naye nyumbani kwao, Oysterbay jijini Dar. 

Amani: Mambo vipi Kajala?
Kajala: Safi kabisa karibu sana nyumbani!
Amani: Leo nimebahatika kumkuta mwanao, kumbe amekuwa binti sasa. 



                                     Paula.
 
Kajala: Hahaha! Si unajua tena leo ni wikiendi mara nyingi nakuwa naye mimi.
Amani: Kwani siku nyingine anakuwa wapi?
Kajala: Anaishi na baba yake hivyo siku ambazo siyo za shule, anakuwa huku kwangu. 

Amani: Hujisikii upweke anapokuwa huko?
Kajala: Siyo kiivyo, nimezoea sababu tangu akiwa mdogo nilikuwa naishi naye mimi kwa hiyo mapenzi ya baba aliyakosa hivyo bora sasa anavyokaa naye inakuwa ni vizuri. 

Amani: Kwa hiyo huko anakaa na baba yake peke yake? 
Kajala: Hapana yuko na bibi yake pamoja na mama yake wa kufikia ambaye anampenda sana mwanangu namshukuru sana kwani ni zaidi ya mama kwa mtoto wangu. 


                               Kajala.
 
Amani: Ulijisikiaje ulivyokuwa mbali na mtoto wako takriban mwaka mmoja na siku kumi ulivyokuwa jela?
Kajala: Hakuna wakati mgumu kama kipindi kile kwani kuna wakati baba yake alimzuia kuja kuniona kwa vile alikuwa anafeli sana nikawa mara nyingi nalia nikimkumbuka. 

Amani: Nini ambacho unakipenda kitokee kwa mwanao?
Kajala: Napenda sana asome sana, asinifuate mimi ambaye sikupenda shule kabisa, maana naamini elimu ndiyo kila kitu katika maisha.

Amani: Nini ambacho hupendi kitokee kwa mwanao?
Kajala: Wanaume wakware wakitaka kumfuata mwanangu kwa kweli sitopenda hata kidogo. 

Amani: Unamzungumziaje Paula?
Kajala: Ni zaidi ya kila kitu kwangu maana yule akikua kidogo tu sitohitaji rafiki zaidi yake. 

Amani: Kajala nakushukuru sana.
Kajala: Karibu tena.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...