Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa pili kulia), akimsilikiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, mhandisi Mussa Nati, alipotembelea kukagua kazi ya ujenzi wa maabara mpya ya shule ya sekondari Manzese jana.
Dar es Salaam. Alifanya Rais Ali Hassan Mwinyi na baadaye Augustine Mrema na sasa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda anataka kufuata nyayo baada ya kutenga kila Ijumaa kuwa siku maalumu ya kusikiliza kero za wananchi wake wa wilaya hiyo kuhusu suala nyeti la ardhi.
Mwinyi, ambaye alikuwa rais wa Serikali ya Awamu ya Pili, alitenga siku ya Ijumaa kuwa maalum kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya wananchi, akitumia ofisi ndogo ya CCM iliyo Barabara ya Lumumba jijini Dar es Salaam.
Na Mrema, ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wakati wa Serikali ya Awamu ya Pili, alitenga siku ya Alhamisi kuwa maalum kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya ndoa.
0 comments:
Post a Comment