UPEPO umegeuka! Imani ya kwamba wanaume ndiyo
wamekuwa wakiwapa kipondo wake zao imegeuka, safari hii mwanamke
aliyejulikana kwa jina la Naomi Peter akimpa kipondo ‘hevi’ mumewe John
Shila mchana kweupe!
Wawili hao wakazi wa Misheni, jijini Mwanza waliibua timbwili la aina
yake ambalo liliwavuta watu wengi chanzo kikiwa ni mwanaume huyo
kumkataa mtoto aliyezaa na mwanamke huyo.
Akizungumza na waandishi wetu, mmoja wa mashuhuda alisema wawili hao
walioana na kuishi kama mke na mume na baadaye kupata mtoto mmoja wa
kike, baada ya miaka miwili ulitokea ugomvi na kusababisha mwanamke
kuondoka na ndipo John alipotumia mwanya huo kuoa mwanamke mwingine.
“Siku ya tukio, Naomi alimpeleka mtoto wake nyumbani kwa mzazi
mwenzake kutokana na kutopewa hela ya matumizi, wakati huo Shila alikuwa
na mwanamke wake mpya ndani, baada ya mabishano ya muda ndipo Naomi
akaanza kumshughulikia Shila kwa kumtandika mangumi.
“Jamaa alikuwa hapeleki matumizi kwa mzazi mwenzie, mbaya zaidi
alikataa na kudai mtoto si wake ndipo timbwili lilipoanzia,’’ kilisema
chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, wakati ugomvi huo ukiendelea
mwanamke wa John wa sasa alikuwa kimya ndani na kushuhudia mpenzi wake
akipokea kichapo kisha kumkabidhi mwanaye amlee na yeye akaondoka zake.
Hadi shuhuda wa habari hizi anaondoka eneo la tukio, muafaka juu ya kilichofikiwa ulikuwa bado haujapatikana.
0 comments:
Post a Comment