2014-12-24

Mambo hayoooo!!! Hivi ndivyo vyama vya siasa vilivyokabana uchaguzi wa mitaa



Image result for NEMBO YA CHADEMA
Fukuto la joto la uchaguzi wa Serikali za Mitaa lilipanda, hasa baada ya wagombea 257 kuzuiliwa kwa kuwekewa pingamizi muda mfupi kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini kote.

Hofu hiyo zaidi ilitawala katika ofisi kadhaa za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), zilizopo katika baadhi ya mikoa, baada ya wagombea wake 228 kuenguliwa kutokana na sababu mbalimbali.

Hali hiyo ilidhihirika zaidi siku moja kabla ya Uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa kufanyika nchini kote, Desemba 14 mwaka huu.

Hali ilivyokuwa katika baadhi ya maeneo

Hatua za mapingamizi zilijitokeza katika mikoa ya Arusha, Manyara na Mwanza ambapo mapingamizi zaidi ya 200 ya Chadema hayakutolewa uamuzi, huku CCM ikipita bila kupingwa katika mitaa na vijiji vingi. 


 Image result for nembo ya ccm



Baadhi ya viongozi na wagombea katika uchaguzi, huo walionya kwamba kutotolewa uamuzi wa rufani za mapingamizi na kuondolewa baadhi ya wagombea, kunaweza kuvuruga uchaguzi huo. 


                        

Hata hivyo, msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arusha, Juma Idd anasema mchakato wa kupitisha wagombea na mapingamizi umekwisha na kilichokuwa kinasubiriwa ni uchaguzi.

Anasema vyama sita vilisimamisha wagombea ambavyo ni ACT kilichosimamisha katika mitaa 11, CCM mitaa 154, Chadema mitaa 154, CUF mitaa mitano, TLP mtaa mmoja na NCCR Mageuzi mtaa mmoja.

Image result for nembo ya cuf



Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Arumeru Mashariki, Gadiel Mwanda alikaririwa akisema wagombea zaidi ya 60 wa jimbo hilo, waliwekewa pingamizi na wao wamekata rufani lakini hawakujua hatima yao.

Katika Jimbo la Monduli, Mwenyekiti wa Chadema, Japhat Sironga anasema pingamizi hizo ni za vijiji vitatu hazikujibiwa na hawakijua hatima yao huku, wagombea wengine wakiamua kujitoa kwenye kinyang’anyiro hicho. 


                                             


Katika jimbo la Simanjiro, mwenyekiti wa Chadema, James Millya anasema kuna upungufu mkubwa katika mchakato mzima na wagombea wake zaidi ya 70 hawajui hatima yao.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...