Msanii wa muziki na filamu Bongo, Simon Mwapagata ‘Rado’.
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Simon Mwapagata ‘Rado’ amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya vibaka kukomba vifaa vya gari lake vyenye thamani ya shilingi milioni tatu.
Akizungumza kwa huzuni juzikati, Rado alisema siku ya tukio alipaki gari lake aina ya Toyota Mark X sehemu aliyoizoea kila siku maeneo ya Mwananyamala na kwenda kulala lakini alipoamka siku iliyofuata na kwenda kulichukua, alikuta site mirror, taa zote, power window na vifaa vingine vimeibwa.
“Yaani nilihuzunika sana baada ya kukuta gari langu liko kwenye hali hiyo huku mlinzi akiwa amelewa chakari halafu hana hata shilingi useme labda anaweza kunilipa, nimeamua kumwachia Mungu maana nikisema nikashtaki watakamatwa watu ambao ni majirani zangu na mimi sitaki ugomvi nao,” alisema Rado.
GPL
0 comments:
Post a Comment