2015-03-24

Sad Nyuzzzzzzzzzz:NDEGE ZA MUUNGANO ZA KIVITA DHIDI YA DAESH ZAUA 66 SYRIA

Ndege za kivita za muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh nchini Syria zimefanya mashambulio katika maeneo kadhaa na kuua raia 66 wa nchi hiyo.
 Harakati ya Kutetea Haki za Binadamu iliyoko nchini Uingereza inayoitwa Syrian Observatory for Human Rights 'SOHM' imeeleza kuwa, raia 66 wa Syria wakiwemo watoto 10 na wanawake 6 wameuawa katika mashambulio yaliyofanywa na ndege za kivita za muungano ulioundwa na Marekani dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh katika mikoa ya al Raqqa, Deir al Zor, al Hassakah, Idbil na mji wa Manjeb ulioko umbali wa kilomita 446 kaskazini mwa Damascus, Mji mkuu wa Syria.

Muungano huo ulianza kufanya mashambulizi ya anga tokea mwezi Septemba mwaka jana ndani ya ardhi za Syria kwa kisingizio cha kushambulia ngome za kundi la kigaidi la Daesh, ambalo limefanya unyama na mauaji makubwa nchini humo.

 Syria ilianza kutumbukia kwenye ghasia na machafuko tokea mwezi Machi 2011, na hadi sasa watu wasiopungua laki mbili na elfu kumi na tano wameshapoteza maisha.
GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...