Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (W) akiongea na waandishi wa habari katika Hoteli ya Atriums kuhusiana na shoo ya Pasaka Dar Live.
Kiongozi wa kundi la sarakasi la Masai Warrios akiongea jambo kuhusu shoo hiyo siku ya Pasaka Dar Live.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akielezea jinsi Vodacom Tanzania ambao ndiyo wadhamini wakuu wa shoo hiyo walivyojipanga.
Mwakilishi wa Kinywaji cha Vita Malt, Bahati Sindi akiongea kuhusiana na shoo hiyo itakayolitikisa jiji la Dar na vitongoji vyake.
10 Wasanii watakaotumbuiza Pasaka Dar Live wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya Hoteli ya Atriums jijini Dar.
Msanii wa kizazi kipya anayetamba na wimbo wa Chekecha Cheketua, Ali Saleh ‘Kiba’ (katikati) akielezea alivyojipanga kutoa burudani ya nguvu katika shoo yake ya Mwana Dar Live itakayofanyika Sikukuu ya Pasaka.
kutoka kushoto, mwakilishi wa Kampuni ya Vinywaji vya Vita Malt, Bahati Sindi akiwa na Isha Mashauzi pamoja na Msaga Sumu katika picha ya pamoja.
Mwakilishi wa Vodacom, Martina Nkuyu akiongea na Msaga Sumu kama wanavyoonekana.
MSANII wa kizazi kipya anayetamba na wimbo wa Chekecha Cheketua, Ali Saleh ‘Kiba’ ametamka kuwa amejipanga vya kutosha anahakikisha anawapagaiwisha mashabiki wake wataojitokeza katika shoo ya Mwana Dar Live siku ya Sikukuu ya Pasaka, Aprili 5 mwaka huu katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani, Dar Live, Mbagala.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hoteli ya The Atriums jijini Dar, Kiba alisema amejipanga vya kutosha kuhakikisha anadondosha bonge la burudani kwa mashabiki wake wataokuja katika shoo hiyo ambapo siku hiyo ataupiga wimbo huo wa Chekecha Cheketua kwa kutumia ‘live’ bendi.
“Nawaomba mashabiki wangu waje kwa wingi kwani siku hiyo nimejipanga vya kutosha kuhakikisha napiga shoo kali ambayo itawapagawisha watu wote ambao watakuja ukumbini hapo ambapo nyimbo zote nitaziimba kwa kutumia vyombo vya jukwaani ‘live band’ .
Naye Mratibu wa Burudani katika Ukumbi huo wa Dar Live, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ amewataka mashabiki wote wapenda burudani wasikose kufika katika ukumbi huo siku hiyo ya Sikukuu ya Pasaka kwani watapata furaha ya kufika ukumbini hapo.
Pia, Isha Mashauzi na Mashauzi Classic pamoja na Msaga Sumu na Masai Warriors watanogesha burudani mbalimbali katika siku hiyo wakimsindikiza Ali Kiba.
0 comments:
Post a Comment