Mama Kanumba akionesha uso wa huzuni baada ya kufika makaburini kwa ajili ya kumkumbuka mtoto wake marehemu, Steven Kanumba.
Ndugu wa mama Kanumba wakiwasha mishumaa.
Kijana aliyekuwa shabiki wa Marehemu Kanumba akiomba, kama ishara ya kumbukumbu yake.
MAMA mzazi wa aliyekuwa msanii nguli wa filamu Bongo Marehemu Steven Charles Kanumba leo mchana aliongoza ibada fupi kama ishara ya kumbukumbu ya kifo cha mwanaye kilichotokea miaka mitatu iliyopita, shughuli iliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Katika hafla hiyo fupi, mama Kanumba akiwa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu, waliwasha mishumaa baada ya kufanya usafi wa eneo la kaburi lake, kumkumbuka nyota huyo aliyefariki Aprili 7 mwaka 2012.
GPL
0 comments:
Post a Comment