Beyonce na Jay Z katika pozi.
MWANAMUZIKI Beyoncé Giselle Knowles 'Beyonce' na mumewe Shawn Corey Carter 'Jay Z' wameripotiwa kuwa kwenye mgogoro tena huku mwanamuziki Rihanna akihusishwa.
MWANAMUZIKI Beyoncé Giselle Knowles 'Beyonce' na mumewe Shawn Corey Carter 'Jay Z' wameripotiwa kuwa kwenye mgogoro tena huku mwanamuziki Rihanna akihusishwa.
Wanandoa hao wapo kwenye mgogoro kutokana na simu ya siri ambayo Jay Z anadaiwa kuitumia kuwasiliana na Rihanna pasipo Beyonce kujua.
Wanaume wengi wana simu za siri ambazo hutumia kuwasiliana na watu wao kwa siri, ila mara nyingi wanakuwa makini kuficha simu zao katika magari yao au kazini.
Kupitia mtandao wa Rhymeswithsnitch.com: Beyonce anadaiwa kumkoromea mumewe Jay Z kwa kuwa na simu ya siri ambayo anatumia kuwasiliana na Rihanna.
Chanzo kimoja cha habari kimeliambia Jarida la Grazia kuwa: “Jay Z ana simu kadhaa ambapo mojawapo ndiyo hutumia kuwasiliana na Rihanna masuala ya kibiashara.
“Ni kawaida anapopigiwa na mrembo huyo, Jay Z hutoka hata nje ya mkutano ili asizuruge vikao, hata akiwa kwenye meza ya chakula akipigiwa simu hutoka nje kuongea na Rihanna.”
Chanzo hicho kimeongeza kuwa Beyonce mwenye miaka 33, anajua kuwa Jay Z ana simu nyingi ila hakujua kama mojawapo ni kwa ajili ya kuongea na Rihanna na anachukia kitendo cha mumewe kuwa karibu na mwanamuziki huyo kutoka Visiwa vya Barbados.
Jay Z mwenye miaka 45, na Beyonce, hivi karibuni walisherehekea miaka saba ya ndoa yao ambapo wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Blue Ivy.
GPL
0 comments:
Post a Comment