Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Shamsa Ford amesema kamwe hatajutia kitendo cha kuachana na mumewe, Dickson.
Akiongea na gazeti la Amani Shamsa alisema kuwa kipindi chote wakati yupo kwenye uhusiano na mumewe huyo waliefunga naye ndo ya kimilia alikuwa akiteseka na kupata shuruba nyingi japo hakuwa tayari kuziweka hadharani.
“Sijutii kuachana na mume wangu, nimepitia mateso mengi, sikotayari kurudi japokuwa nina motto naye” Shamsa alisema.
Kwa sasa inadaiwa Shamsa anatoka na Staa wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego ambaye naye aliachana na mchumba wake ,Siwema hivi karubuni.
0 comments:
Post a Comment