2015-04-08

ROSE NDAUKA USIMTAFUTE MCHAWI KWENYE MATUKIO YAKO MABAYA!

Mwigizaji maarufu wa sinema za kibongo, Rose Ndauka.

KWAKO mwigizaji unayezitendea haki sinema za Kibongo, Rose Ndauka. Mambo vipi dada yangu? Habari za siku nyingi? Kitambo kidogo hatujaonana, nafikiri ni kutokana na majukumu yetu kuwa mbalimbali.

Ukitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima nashukuru Mungu maisha yanasonga kama kawaida, naendelea kusukuma gurudumu la maendeleo na moja ya majukumu yangu ya kila siku ni kuwakumbuka mastaa kwa njia ya barua kama nilivyokukumbuka wewe leo hii. 

Madhumuni ya barua hii ni kutaka kukukumbusha juu ya majukumu yako kama staa na mambo ambayo unapaswa kuyafanya kama msanii. Sisi kama waandishi tuna haki ya kuandika kitu chochote kinachohusiana na kazi zenu na hata maisha yenu ya kila siku.

Ukishakubali kuwa mwigizaji jua kwamba wewe si sawa na mimi au na jamaa flani anayeishi kule mtaani. Jua kwamba watu wanataka kujua unafanya nini, unaishi vipi na hata unavaa nini na kwa wakati gani.
Watu wanataka kuishi kama unavyoishi wewe, wanataka kuwa kama wewe katika vitu mbalimbali ambavyo wanavutiwa navyo kutoka kwako.

Ukifanya vitu vya ajabu, watu watakushangaa maana wanategemea kuona vitu vizuri kutoka kwako na si vibaya.
Hapo ndipo umuhimu wetu unapokuja. Tupo kwa ajili ya kuwajuza wananchi kile mnachokifanya kila kukicha.
Ndiyo maana uliona tumeripoti sana kazi zako tangu unaanza sanaa hadi kufikia hapo ulipo. Tuna mchango mkubwa wa kukutangaza na kutengeneza jina lako, najua huwezi kubisha labda uwe mjeuri.

Juzi nilisikitishwa na wewe kujifanya unakanusha habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Amani iliyokuwa inakuhusu wewe kuwa na uhusiano na prodyuza Manecky wa AM Records.Kwanza unapaswa kuelewa sisi huwa hatukurupuki kuandika habari. Tunachokiandika lazima kiwe na ukweli hivyo kukanusha kwako hakukuwa na maana yoyote. 


Kama uliona kuna tatizo lolote la kiuandishi, ulipaswa kutujuza na si kuwahadaa watu kwenye mitandao ya kijamii ili uonekane msafi wakati ukweli kuhusu jambo hilo unaujua na ndiyo maana hata huyo mwenzako hakukanusha.

Mwenzako anajua vyombo vya habari ni nini. Hakurupuki hata siku moja. Global Publishers siku zote haiandiki kitu ambacho hakipo, lazima kiwepo. Ndiyo maana tuliripoti migogoro kuhusu kusuasua kwa uchumba wako na Malick Bandawe hadi kufikia hatua ya kuyeyuka.

Nikusihi dada yangu, achana na kukanusha habari ambazo unajua moyoni kuwa zina ukweli. Usijifanye mwema wakati nyuma ya pazia sivyo, siku zote sisi tunasimamia weledi.Ukiwa msafi tunaripoti usafi wako na ukiwa mchafu pia hatutaacha kuandika.Bila shaka umenielewa, kwa leo acha niishie hapo, naomba ubadilike!
GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...