2015-04-08

Ni sheeeeeeeeeedah!!!!!!!!!! SHILOLE AFANYA ‘UTUNDU’ STEJINI

 Mwanadada Shilole 'Shishi Baby' akionyesha mbwembwe zake stejini na mmoja wa mashabiki wake.
STAA wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Zuwena Mohamed 'Shilole' juzikati aliwatega vidume baada ya kufanya utundu wa aina yake kwa kuwaita jukwaani na kucheza nao wakati akipafomu kwenye shoo maalum ya Pasaka iliyodhaminiwa na Vodacom mwishoni mwa wiki. 

Tukio hilo lilinaswa sawia na paparazi wetu maeneo ya Coco Beach jijini Dar es Salaam baada ya Shilole kupandwa na ‘mzuka’ wakati akicheza na madensa wake waliovaa vibukta vifupi ambapo aliwaomba wanaume kadhaa wapande jukwaani wacheze naye kwa staili za ‘hatari’ kwani yeye alilala chini na mwanaume akaja kwa juu, hali iliyozua miguno kwa umati uliohudhuria. 

 

Shilole akizidi kupagawisha mashabiki wake.

“Jamani hebu mwangalieni Shilole vitendo anavyovifanya pale jukwaani yaani dah, anajua kabisa hii shoo hata watoto wadogo wapo, hapo sijui anawafundisha nini, mimi sijapenda kabisa,” alisikika akilalamika shabiki mmoja.
 

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...