Kombora la Balestiki.
JESHI la Anga la Marekani limetangaza kuwa limefanyia majaribio kombora la Balestiki linaloweza kuvuka mabara na kwamba majaribio hayo ni ujumbe kwa walimwengu kuhusu uwezo wa silaha za nyuklia wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Anga la Marekani, kombora la Minuteman-III lilifanyiwa majaribio mapema Jumatatu katika kituo cha Jeshi la Anga cha Vandenberg huko California. Taarifa ya Jeshi la Anga la Marekani imesema: Majaribio hayo ya kombola la balestiki la nyuklia yanaonesha picha ya wazi kwa walimwengu kuhusu uwezo wa kombora ya Minuteman-III ambalo linaweza kulenga mahala popote.

Kombora la Balestiki linavyolipuka.
Kwa kutilia maanani kwamba Jeshi la Anga la Marekani haliwezi kutumia makombora ya Peace Keeper kwa mujibu wa makubaliano ya silaha ya START II (Strategic Arms Reduction Treaty), kombora la Minuteman-III litakuwa kombora pekee la balestiki linaloweza kuvuka mabara la jeshi la Marekani. Kombora hilo linavishwa kichwa cha silaha ya nyuklia aina ya W87 ambacho kina uwezo mkubwa wa uharibifu. Majaribio hayo yamefanyika sambamba na mazoezi ya kijeshi yanayoendelea kufanywa na majeshi ya shirika la NATO huko Ulaya mashariki.
Inaonekana kuwa kwa majaribio ya kombora hilo la nyuklia, jeshi la Anga la Marekani linafuatilia malengo kadhaa.
Kwanza ni kuwa Marekani inataka kuonesha misuli na uwezo wake wa silaha za nyuklia kwa wapinzani wake wakubwa hususan Russia. Katika kipindi cha miaka kama miwili iliyopita jeshi la Russia limefanya majaribio mtawalia ya makombora yanayoweza kuvuka mabara (Intercontinental Ballistic Missile au IBM) na hata kurusha makombora kama hayo kwa kutumia nyambizi. Kwa msingi huo Marekani ilikuwa ikinyemelea fursa ya kukabiliana na majaribio hayo ya silaha za nyuklia ya Russia.
Suala la pili ni kushadidi mivutano baina ya Russia na NATO huko Ulaya Mashariki ambako kumezifanya pande hizi mbili zijizatiti kwa silaha na majeshi katika eneo hilo na katika Bahari Nyeusi. Kwa msingi huo Marekani inataka kumuonesha adui wake yaani Russia, kwamba iwapo mgogoro huo utaendelea inaweza kutumia silaha zake za nyuklia.
Marekani ni miongoni mwa wamiliki wakubwa zaidi wa silaha za nyuklia duniani na ndiyo nchi pekee ambayo hadi sasa imetumia silaha hizo kuua watu wa taifa jingine. Nchi hiyo kinyume na ahadi zake za kupunguza maghala yake ya silaha za nyuklia, ingali inastawisha na kupanua zaidi silaha hizo na kuzifanyia majaribio.
Marekani pia inasasisha na kuziboresha zaidi silaha zake za zamani za nyuklia licha ya harakati za kimataifa za kupunguza silaha hizo husuan mkataba wa NPT unaosisitiza kupunguzwa na hatimaye kuangamizwa kabisa silaha hizo. Katika uwanja huo Washington imetenga bajeti ya dola bilioni 355 ambazo zitatumika kusasisha na kuboresha mitambo yake ya silaha na kuinua juu kiwango cha majaribio ya silaha za nyuklia. Vilevile Marekani imechukua hatua za kuboresha silaha na maghala yake ya zana za nyuklia barani Ulaya yakiwemo mabomu ya nyuklia ya B-61.
Kwa utaratibu huo, Washington, kinyume na mikataba ya kimataifa ya kuzuia uzalishaji wa silaha za nyuklia, inaendelea kuzalisha na kufanyia majaribio silaha za aina hiyo, suala ambalo linakiuka mkataba wa NPT.
0 comments:
Post a Comment