2014-12-31

MIMBA YA AUNT YAONYWA NA DOKTA

1
TABIA za mitoko ya usiku matembezini, uvaaji viatu virefu na unywaji pombe unaofanywa na wamama wajawazito, kama alivyo sasa muigizaji Aunt Ezekiel, zimeelezewa kuwa si nzuri na zina uwezekano mkubwa wa kusababisha madhara kwa mtoto anayetarajiwa kuzaliwa. 


Mkali katika tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
Akizungumza baada ya kuulizwa na gazeti hili juu ya mwenendo wa muigizaji Aunt Ezekiel ambaye mara kadhaa huonekana akiwa ‘viwanja’ usiku, daktari mtaalamu wa magonjwa ya kina mama na watoto, aliyejitambulisha kwa jina moja la Dokta Chale, alisema utokaji wa usiku na uvaaji wa viatu virefu unaweza kusababisha matatizo ya nyonga, shida wakati wa kujifungua, miguu kuuma na uvimbe kwenye vifundo vya miguu ‘enka’. 


Kuhusu unywaji pombe, Dokta Chale alisema endapo mama mjamzito atafanya tabia hiyo, ipo hatari ya uelewa wa mtoto katika ukuaji wake kuwa mdogo na pia kuchukua tabia zote za mama yake.



...Akizidi kujiachia.

“Viatu virefu na mitoko ya usiku kwa mama mjamzito ina madhara makubwa sana kwani mtoto atakuwa na uelewa mdogo, yaani akili yake inakuwa haikui sawasawa, kifupi ana-adapti (kuiga) tabia zote za mama yake anaweza kuwa zezeta kama mama anatumia pombe,” alisema. 


Katika kudhihirisha kuwa ustaa ni kazi kubwa, licha ya ujauzito wake kuonekana mkubwa, Aunt Ezekiel amekuwa akijirusha kama kawaida sehemu mbalimbali nyakati za usiku huku wakati mwingine akiwa amevaa viatu virefu.

Ina sikitisha sanaaaaaa!!!!!!!!! Boko haram wavamia kijiji na kuua 15




 
Wapiganaji wanaodhaniwa kuwa ni Boko Haram wamevamia kijiji Kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuua watu takriban 15.

Shambulizi hilo lilitokea katika kijiji cha Kautikari katika jimbo la Borno, pale washukiwa wa Boko Haram walipowasili kijijini humo kwa magari yenye silaha, wakilenga askari wa ulinzi wa jadi wa mji huo.


Kijiji hicho kipo karibu na Chibok mahali ambapo kundi la Boko Haram, liliwateka nyara wasichana wa shule zaidi ya mia mbili mwezi Aprili mwaka huu.

Zaidi ya watu elfu kumi wameuwawa Nchini Nigeria na Boko Haram mwaka huu pekee.

MISS TANZANIA HUNDI YAWAPONZA




Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema moja ya sababu ya kufungia mashindano hayo ni waandaaji, Kampuni ya LINO kutoa hundi feki ya malipo ya kibali ya Sh2Milioni. 

BARAZA la Sanaa na Taifa (Basata) jana Jumatatu lilitoa sababu za kuyafungia mashindano ya Miss Tanzania kwa miaka miwili ikiwemo Kampuni ya LINO kuwasilisha hundi feki katika baraza hilo. 

Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema moja ya sababu ya kufungia mashindano hayo ni waandaaji, Kampuni ya LINO kutoa hundi feki ya malipo ya kibali ya Sh2Milioni. 
 

“Walituletea hundi muda mfupi kuelekea siku ya shindano tukawaamini lakini kumbe ilikuwa feki na hadi leo leo hawajalipa,” alisema. Mkurugenzi wa LINO, Hashimu Lundenga alisema: 
“Basata walichelewa kuipeleka benki hundi tuliyowapa, lakini tunakiri ilikuwa na makosa na tumekubaliana tutawali

MISHEMISHE ZA KUMPOSA MCHUMBA WAKE ZAMTOKEA PUANI


'Kreni' ilitumbukia ndani ya nyumba wakati ikimbeba mwanamume aliyekuwa anamposa mpenzi wake 

Mwanamume mmoja raia wa udachi amejikuta akikimbilia usalama wake baada ya jaribio la kutaka kumposa mpenzi wake kwa mbwembwe kwenda mrama. 

Mtu huyo ambaye hakutajwa kwa jina anayeishi mjini Ijsselstein alikodisha 'kreni' au Crane na kuipanda akipanga kwamba kreni hilo imtoe chini na kumpanidhs hadi dirishani mwa mpenzi wake ambapo angemchezea wimbo na kisha kumposa. 

Badala yake yaliyomkuta hakuyatarajia kabisa.Kreni hiyo ilianguka chini na kupita dirishani kwa mpenzi wake huku ikiangukia nyumba za majirani. 


Mwanamume huyo alilazimika kukimbilia usalama wake na hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo lililowaacha wengi wakiangua kicheko.

Kwa mujibu wa jarida la Algemeen Dagblad, mpenzi wake mwanamume huyo alimkubali na kusema yuko radhi kuolewa naye licha ya tukio hilo.

Baada ya kuongea na polisi, wawili hao walisafiri kwenda mjini Paris Ufaransa kusherehekea. 


Kreni hio ilianguka tena kwa mara ya pili ilipokuwa inainuliwa na hata kuharibu zaidi nyumba za majirani. Meya wa mji huo, amezomewa na wengi baada ya eneo hilo kusemekana kutokuwa salama.

INA HUZUNISHA SANAAAAA!!!!!!! WEMA KUUMALIZA MWAKA KWA KILIO!



Mkali katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam akilia huku akibembelezwa na shost yake Aunt Ezekiel. 

OHOOOO! Wakati pazia la mwaka 2014 likifungwa leo, mama la mama, Wema Sepetu ‘Madam’ ameuaga mwaka huo kwa staili ya kilio cha nguvu, mchapo hatua kwa hatua huu hapa... 


Tukio hilo lililozua maswali mengi bila majibu, lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 29, mwaka huu kwenye shoo ya Madam ya kuuaga mwaka 2014 (Say Good Bye To 2014) iliyofanyika katika Klabu 71, Tegeta-Kibaoni jijini Dar.

Kabla ya kukutwa na kisanga hicho kwenye shoo hiyo ambayo Madam aliiandaa chini ya Kampuni yake ya Endless Fame, shoo mbalimbali kutoka wasanii kibao wa Bongo Fleva kama Barnaba, Izo Business, Bob Junior na wengine wengi zilihusika kisha baadaye Wema alipanda jukwaani na kumtambulisha msanii wake mpya ajulikanaye kwa jina la Ally Luna. 

“Ally Luna atasimamiwa shughuli zote za kimuziki na mimi chini ya kampuni yangu Endless Fame, na atapata huduma zote za muhimu kama inavyofanyika kwa msanii wangu wa zamani, Mirrow,” alisikika Wema. 
 

Mara baada ya shoo hiyo iliyoambatana na bethidei ya mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown kumalizika, Wema alikutwa na mapaparazi nje ya ukumbi huo akiangua kilio cha nguvu ambacho hakikujulikana moja kwa moja ni cha nini

2014-12-30

TUNAENDA WAP TANZANIA;MWANAMKE ADAIWA KUTEKA WATOTO


Mama anayefahamika kwa jina la Sara Zoya akiwa na watoto wake, Imani (14) na Leila (5). 



Mama mmoja, Sara Zoya mkazi wa Mabibo Makuburi, jijini Dar es Salaam amekimbilia polisi na kudai kuwa watoto wake walitekwa na ndugu yake kisha kupelekwa kusikojulikana baada ya kufukuzwa kwenye nyumba yao ya familia.

Sara alidai kuwa ndugu yao huyo aliyefanya kitendo hicho cha utekaji ni Hilda Zoya ambaye anadai aliwateka watoto Imani (14) na Leila (5).

Akizungumza na gazeti hili Sara alisema, alikuwa akiishi na mumewe na baada ya kuachika kwa mume wake aliamua kurudi kwao kwenye nyumba ya familia na watoto hao wawili. Aliendelea kufafanua: 
 


“Sisi tulizaliwa watoto sita kwa baba na mama mmoja na mimi ndiye mtoto wa kwanza na wazazi wetu wote walishafariki dunia. Mimi nilipoachika niliwataarifu ndugu zangu kuwa nataka kurudi nyumbani kwetu Mabibo lakini baadhi yao wakanishauri niende nikakae Tabata Kisukuru kwenye nyumba ya mdogo wangu anayeishi Ulaya.

“Mimi sikupenda, nikakataa nikaenda kuishi kwetu, ilipofika Desemba 17 mwaka huu, ndugu yangu Rachel kutoka Ulaya aliyekuja likizo aliniomba nimsindikize kwa mjomba anayeishi Mbezi Beach huku nyuma mdogo wangu Hilda alihamisha vyombo vyote na kuwachukuwa watoto na kuwapeleka kusikojulikana.
“Niliporudi nyumbani nilikuta milango imefungwa na vitasa vimebadilishwa na kuwekwa mlinzi pia watoto wangu wawili sikuwakuta.

“Nikaenda kwa mjumbe, mwenyekiti wa serikali za mitaa kuwaarifu na baada ya hapo nikaenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi cha Mwongozo kilichopo External, wakaniambia nisubiri kwa muda wa saa 24 lakini sikuwaona wanangu na mama yao mdogo Hilda alikuwa hapatikani kwenye simu, ndipo nikaamua kurudi tena kituoni hapo na kufungua kesi kuhusu kutoonekana kwa watoto, vitu vyangu na mimi kukosa pa kulala.”

Sara amemfungulia kesi mdogo wake Hilda kwa jalada namba MWP/RB/1655/2014 UTEKAJI WA WATOTO NA WIZI hivyo anasakwa na polisi.Akifafanua zaidi mama huyo alisema: “Siku ya pili watoto walirudi wenyewe na walipohojiwa walidai walipelekwa Kinondoni kwa Manyanya na mama yao mdogo na kutelekezwa huko na aliwaachia shilingi elfu tano.

“Watoto walisema walipoamka asubuhi waliwauliza wapangaji wa nyumba hiyo wapi walipo na wakaelekezwa kuwa pale ni Kinondoni kwa Manyanya.”

Mtoto Imani alipoulizwa na gazeti hili alikiri kuchukuliwa na mama yao mdogo na kutelekezwa Kinondoni. “Asubuhi tuliwaomba wapangaji watuelekeze namna ya kufika stendi, tukapelekwa tukapanda basi mpaka Makumbusho kisha tukafika nyumbani, tukaelezwa kuwa mama alilala kwa mwenyekiti wa serikali za mitaa.”

Sasa Sara anaomba msaada wa kisheria kwani alidai yeye pamoja na watoto wake hawana nguo, vyombo na sehemu ya kuishi baada ya kufanyiwa unyama huo na mdogo wake huyo na sasa wamefadhiliwa na mwenyekiti wa serikali za mtaa wanakoishi.

AME FUNGUKA;LICHA YA KUSHUTUMIWA KATIKA SAKATA LA ESCROW MUHONGO AKEMEA RUSHWA TANESCO






Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Surubu, Kata ya Komaswa wakati wa ziara yake wilayani Tarime Mkoa wa Mara.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewataka wananchi wa vijiji vya wilayani hapa kutoa taarifa za mianya ya rushwa wakati wanapoomba kuunganishiwa umeme majumbani.Muhongo alisema hayo juzi alipokuwa akikagua awamu ya pili ya Mradi wa Umeme Vijijini unaoendelea kwa nchi nzima na ambao mkoani Mara unatekelezwa katika vijiji 197.Alisema katika mradi huo, Serikali haitamwonea huruma mfanyakazi yeyote wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) atakayebainika kuomba rushwa ili atoe huduma. 


“Msitoe hongo,” alisema Profesa Muhongo. “Kati ya vitu ambavyo Serikali haitaki kuvisikia ni rushwa. Msidanganywe kuwa mkitoa rushwa ndiyo mtarahisishiwa kupata umeme kwa haraka.”

Alisema gharama zote za kuunganishiwa umeme kwa mwanakijiji zinalipwa na Serikali na kiasi cha Sh27,000 ni tozo ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (Vat).

Baadhi ya watu walilalamika kuwa mradi huo unawanufaisha wakazi wachache walio jirani na barabara zinakopita nguzo za umeme na kuacha maeneo yaliyo na watu wengi na huduma za kijamii kama shule na zahanati.

“Huduma inayotolewa na ofisi za Tanesco katika wilaya hii ni mbovu sana na mradi huu unapita mbali na makazi ya wanakijiji wengi. Tunaomba utusaidie ili tupate huduma bora,” alisema mkazi wa Bunda, Sherida Charles.

Naye kaimu mkuu wa wilaya hiyo, Angelina Mabula aliwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kuunganishiwa umeme ambayo alisema ni chachu ya maendeleo katika sekta mbalimbali hasa ya afya na elimu.

“Hivi sasa kuna ujenzi wa maabara za kisasa katika shule zetu, haziwezi kufanya kazi bila umeme,” alisema Mabula.

Mabula alisema vikiunganishiwa umeme, vituo vya afya vitaondokana na adha ya wauguzi kuhangaika na vibatari wanapotoa huduma, hususan kwa wajawazito.

“Watakuwa pia wamejikomboa kutembea umbali mrefu kutafuta huduma bora na salama na hakutakuwa na haja ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo,” alisema Mabula.
Aidha aliwataka wananchi kulinda miundombinu ya umeme hasa wale walio zoea kuiba mafuta ya Transifoma na nyaya kwa makusudi ya kuuhujumu uchumi wananchi

MAMBO MOTO; BILLIONEA MWANAMKE MWEUSI TAJIRI ZAIDI DUNIANI_AMPIKU OPRAH WINFREY



Bilionea wa Nigeria, Folorunsho Alakija amempiku Oprah Winfrey kama mwanamke mweusi tajiri zaidi duniani kwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 7.3 kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na jarida la Ventures Africa. Bilionea wa Nigeria, Folorunsho Alakija amempiku Oprah Winfrey kama 
mwanamke mweusi tajiri zaidi duniani kwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 7.3 kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na jarida la Ventures Africa. 

Oprah ana utajiri ufikao dola bilioni 2.9 kwa mujibu wa Forbes. Hata hivyo orodha ya hivi karibuni ya Forbes ilionesha kuwa Alakija ana utajiri wa dola bilioni 2.5.
Utajiri wa mwanamke huyo umetokana na biashara ya mafuta na anamiliki visima vingi vya mafuta nchini Nigeria.

2014-12-29

Hongera Messi kupewa tuzo ya heshima


Chama cha soka cha Hispania (LFP) kimetangaza kitampa Lionel Messi tuzo ya heshima kwa kuvunja rekodi ya ufungaji bora wa la liga kwa muda wote.


Messi amevunja Rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Telmo Zarra ya kufunga Bao 251 alipofunga mabao matatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Sevilla.

Rais wa chama cha soka cha Hispania Javier Tebas, amethibitisha kuwa watatoa tuzo hiyo kwa mshambuliaji huyo wa timu ya Barcelona.


Messi atapewa Tuzo hiyo Januari 11 katika Uwanjani Nou Camp wakati Barca itakapocheza Mechi ya Atletico Madrid.

Mpaka sasa Messi, amekwisha funga jumla ya mabao 258 katika ligi ya Hispania, huku hasimu wake wa karibu Cristiano Ronaldo akiwa nafasi ya tisa katika historia ya ufungaji bora wa muda wote.

Aliye Taka KuongozaNchi Afa akitafuta urais 2015



Ni utabiri wa mtoto wa Sheikh Yahya Hussein.Alhaj Maalim Hassan Yahya Hussein.



Mrithi wa Mnajimu na Mtabiri wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Marehemu Sheikh Yahya Hussein, Alhaj Maalim Hassan Yahya Hussein, ametabiri kwamba kiongozi mmoja mzee aliye kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais, atadondoka ghafla kwenye jukwaa na kufa mwakani.

Amesema kiongozi huyo, ambaye hakumtaja jina, atafariki dunia baada ya tukio hilo wakati akikimbizwa hospitali.

Alitangaza utabiri huo, alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana, kuhusu kutumia kwa utabiri alioutangaza mwaka 2014, uchaguzi mkuu na utabiri wa mambo mbalimbali yatakayotokea mwaka 2015.

“Kiongozi mmoja mzee kwa umri ambaye yumo kwenye sakata la urais atadondoka ghafla kwenye jukwaa na kufa akikimbizwa hospitalini,” alisema Maalim Hassan.

Pia alisema kwa mwaka mpya wa 2015 kuanza siku ya Alhamisi, kunaashiria wazee maarufu na hasa wale walio katika uongozi au waliokuwa viongozi kufariki kwa wingi na kwa hilo akasema: “Mtaona ajabu yake.”

Vilevile, alitabiri mwaka 2015 kwamba utakuwa wa shida kubwa kwa familia, ambazo iwapo wahusika hawatafanya juhudi za kuangalia watoto wao, vifo vya ajabu vitatokea ndani ya familia zao.


Pia alitabiri mwaka 2015, wizi utakuwa mwingi na wezi watauawa na udhalimu wa madhalimu utabainika na kuumbuka.

Aidha, alitabiri mwaka 2015 kushuhudia uongo mwingi wa kutisha hasa kutoka kwa viongozi wa kidini na kisiasa pamoja na wanawake wenye nyadhifa au maarufu katika jamii

Pia alitabiri mwaka 2015 utamweka wazi kiongozi mmoja mashuhuri wa siasa nchini kurukwa kwake kwa akili bila kufichwa au kusitiriwa kama ilivyokuwa katika mwaka 2014.

Alisema katika mwaka 2014, kiongozi huyo alikumbwa na mkasa huo, lakini suala hilo likafanywa kuwa siri kubwa.

Pia alitabiri misiba miwili ya kitaifa kutokea nchini mwaka 2015 kwa mujibu wa nyota na kwamba, kuna kiongozi mmoja wa kidini atakumbwa na kashfa ya mwaka itakayomsababishia anguko kubwa na la aibu.

Kadhalika, alitabiri viongozi wawili wa siasa na dini kwamba watakumbwa na kashfa ya ngono, ambayo itawasababishia anguko la utumishi wa kutukuka na familia zao.

Pia alitabiri mwandishi mmoja mashuhuri nchini atakumbwa na umauti wa utata utakaoitesa serikali na familia yake kutafuta suluhu.

Alisema mwaka 2015 utakuwa wa viongozi kuzama kisiasa na kukumbwa na kashfa kubwa zitakazowaondoa madarakani, ikiwa na maana kwamba viongozi wanaofahamika wataanguka kiuchumi, kisiasa, kibiashara na kijamii.

RAIS AJAYE
Pia alitaja sifa za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakayepatikana baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ambazo kwa kiasi kikubwa zinamlenga Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.

Alisema mwenye sifa hizo, ndiye atakayekuwa Rais pekee mwenye nyota ya kudumisha sifa ya Tanzania ya amani na utulivu kwa kuwa mwaka 2015, utaanza siku ya Alhamisi, ambayo kinyota hutawaliwa na sayari ya Mushtara (Jupiter) yenye nyota za Mshale na Samaki.

Maalim Hassan alisema Rais pekee mwenye nyota hiyo, ana sifa ya kuwa kijana mwenye mchanganyiko wa dini mbili za wazazi na/au ndoa za dini tofauti.

“Natabiri kuwa ili Tanzania iepukane na majanga yenye dhamira ya kuifutia sifa yaje ya utulivu na amani duniani, Rais pekee mwenye nyota ya kulizuia hilo kutokea ni kijana mwenye mchanganyiko wa dini mbili za wazazi na/au ndoa za dini tofauti,” alisema Maalim Hassan.

Hata hivyo, baadhi ya waandishi wa habari walimweleza Maalim Hassan kuwa sifa hizo zinamlenga moja kwa moja January, hivyo wakataka kujua sababu za nyota kutokutaja kabisa jina la kiongozi huyo.

Akijibu swali hilo, Maalim Hassan alisema yeye hajui watu waliotangaza azma ya kutaka kugombea urais.

Alisema zaidi ya hivyo, miongoni mwa aliowasikia wakitangaza yumo pia Hamisi Andrea Kigwangallah, Mbunge wa Nzega (CCM), ambaye majina yake yanaonyesha kuwa yanatokana na dini tofauti.

Maalim Hassan alisema atataja rasmi jina la Rais ajaye ifikapo Machi, mwakani na kwamba, kwa sasa nachokifanya ni kuonyesha mwelekeo wa kiongozi huyo mkuu mpya wa nchi.

January, ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli (CCM) ni kijana mwenye umri wa miaka 41, ana mchanganyiko wa dini mbili za wazazi.

Baba yake mzazi, Yusufu Rajab Makamba ni muislamu na mama yake mzazi, Josephine ni Mkristo wa madhehebu ya Katoliki.

Maalim Hassan alisema nyota hizo za mwaka 2015 kwa Tanzania ikizingatiwa kuwa mwaka huo ndiyo wa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, zinaashiria kwamba, mafanikio makubwa yatakwenda kwa vijana ambao ndiyo wenye uwezo wa kwenda kwa kasi ya nyota ya Mshale na kukabiliana na mabadiliko yanayotarajiwa kutokea.

Alisema wale watakaofanikiwa katika mwaka huo, watakuwa ni vijana ama kwa umri wao, sura zao, matendo yao au uvaaji wao.

“Kwa kuwa Tanzania imegawanyika kwenye makundi mawili ya wanaowania kiti cha urais vijana na wazee, nyota zinaonyesha kuwa watakaonufaika kinyota watakuwa ni vijana,” alisema Maalim Hassan.

Hata hivyo, alisema kuna wazee pia wanaweza kufaidika, ambao ni wale watakaokuwa na sura au wenye kupenda mambo ya ujna na kusiriki kusaidia vijana.

Aliwashauri vijana wasiokuwa na sura za ujana wala kupenda au kujishughulisha na mambo ya ujana na kuonekana ni wakubwa kuliko umri wao, hao wajitambue kuwa mwaka 2015 siyo wao na ni vyema wakajiondoa mapema kupeka kuanguka na kuumbuka kwa kiwango cha hali ya juu.

Alisema kwa mujibu wa sayansi ya nyota, hali hiyo hujirudia kila baada ya kati ya miaka 50 na 55.

“Historia inaonyesha hapa kwamba miaka 54 iliyopita Mwalimu Julius Nyerere alikuwa kijana na ndiye aliyeshinda uchaguzi mkuu wa kwanza wa Rais Tanzania Bara, huku wazee mashuhuri wakikubali kukaa pembeni na kuwaachia vijana kuongoza nchi.

Alitabiri mwaka 2015 nyota ya Rais Jakaya Kikwete kwamba, itazidi kung’ara kama ilivyokuwa kwa mwaka huu.

Alisema pia tishio la nchi wahisani kuiwekea Tanzania vikwazo vya kiuchumi litalegezwa na kuifanya nchi kuingia kwenye uchaguzi mkuu wake kwa staha.

Alitabiri kupatwa kwa jua kwa mara ya kwanza, kutatokea Machi 20, 2015 siku ya Ijumaa.

Pia alitabiri fujo, ghasia, vifo, uadui, mauaji na usaliti mkubwa miongoni mwa wananchi na wapendwa wao kwenye uchaguzi mkuu ujao wa rais, wabunge na madiwani.

Vilevile, Jeshi la Tanzania litatumika kitaifa na kimataifa kuzima machafuko ya ndani na nje ya nchi, ambayo yatatokea na kwamba, mwaka 2015 utakuwa wa mafuriko na dhoruba vitakavyoleta madhara makubwa nchini na nje ya nchi na kushauri tahadhari kuchukuliwa kuepuka madhara hayo.CHANZO: NIPASHE

MAMBO MAPYA; ATM YA NBC YAZINDULIWA

Meneja wa ATM na Kadi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Wambura John (kushoto) akiweka pesa kwa kutumia ATM katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya kuweka pesa (deposit) kwa kutumia mashine za ATM ya benki ya NBC jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni mteja wa benki hiyo, Francis Xavier na kulia ni Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter
Mteja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Francis Xavier (kushoto) akiweka pesa (deposit) katika mashine ya ATM ya benki hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Meneja wa ATM na Kadi wa NBC, Wambura John (katikati) na Meneja Huduma za Jamii wa benki hiyo, Irene Peter.



BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma mpya ya kuweka fedha kwenye mashine za ATM jijini Dar es Salaam katika juhudi za benki hiyo kuboresha huduma za kifedha nchini.

Kuanzishwa kwa huduma hiyo kunathibitisha malengo ya benki hiyo ya kutoa huduma sahihi na ya wakati kwa wateja wake nchini nzima na huduma hii ya kuweka fedha kwenye mashine za ATM itakuwa ikipatikana masaa 24 kila siku. Vijimambo

Ameamua Kusema; SlaaJK awaombe radhi Watanzania



SLAA



Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete, kuwaomba radhi Watanzania kwa madai ya kuingizwa kwa wawekezaji wasiojali maslahi ya wazalendo.

Kutokana na hilo alisema kuna uwezekano wa kuwapo kwa kashfa nyingine zaidi ya ile ya akaunti ya Tegeta Escrow katika eneo la Magereji, barabara ya kwenda Wazo Hill, jijini Dar es Salaam kwa madai ya mwekezaji kuwanyang’anya eneo la shughuli za ufundi wa magari wakazi wa Kata ya Wazo takribani 4000 na vijana ambao wamewekeza kiasi cha Shilingi bilioni 35 kwa maendeleo yao ya ufundi wa magari kwenye eneo hilo.


Dk. Slaa alitoa kauli hizo wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mkanada jijini humo jana kwa lengo la kuwashukuru wakazi wa kata hiyo kwa uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika hivi karibuni na hivyo kuelezwa kero hizo ambazo wananchi hao wanakabiliana nazo ikiwa ni pamoja na eneo hilo kudaiwa kutwaliwa na mwekezaji huyo na kuwaondoa vijana hao kwa bati 20 na mifuko ya saruji 20.


Dk. Slaa alisema kuwa wawekezaji wazuri ni wale wanaohakikisha wazalendo wananufaika na wao pia na siyo kuwa wauaji na wasiojali utu wa watu akisema hiyo ni Escro nyingine zaidi ya ile ya uchotwaji wa mabilioni ya Shilingi.

“Haiwezekani watu wamewekeza kwa bilioni 35 wewe unawatoahalafu unawapa mifuko kumi ya saruji na mabati 20,” alisema Dk. Slaa.

Alisema kutokana na hilo, Rais awaombe samahani Watanzania huku akihoji kwamba inakuwaje Rais Kikwete tangu atangaze kuwapo kwa majina 40 ya wanaouza dawa za kulevya na wanaosafirisha wanyama nchi za nje, lakini hadi sasa hajayaweka wazi kwa wananchi.

Aliongeza kuwa, hotuba ya Rais Kikwete kwa wazee wa Mkoa wa dare s Salaam Jumatatu iliyopita ilikuwa na udhaifu mkubwa kwani dhahiri ilionyesha kumtetea mmiliki mpya wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Herbinder Sethi, bila kuangalia maslahi ya taifa.

Dk. Slaa pia alimtaka Rais Kikwete kuwashughulia baadhi ya viongozi ndani ya CCM wanaodaiwa kuhusika kwenye biashara ya kusafirisha wanyama.
Baadhi ya wakazi hao walidai kuwa, sakata la mgogoro wa mpaka wa ardhi katika eneo la Chasimba, bado bichi kwani wananchi hao walitaka kuondolewa kwa utapeli.

Wakazi hao wana mgogoro wa muda mrefu na kiwanda cha Saruji cha Wazo baada ya kudaiwa kuwa walilivamia eneo hilo.

Walisema katika awamu ya kwanza walitaka kuwahamishia eneo la Bungu kwa Masista watu 1,000, lakini baadaye waligundua kuwa eneo hilo kwa mujibu wa ramani za mipango miji liliwekwa kwa ajili ya shughuli za biashara, nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa na kwa ajili ya nyumba wakubwa.

Hata hivyo, wakazi hao walipohoji kuhusu hilo na watu wengine 3500 kwamba watawapeleka wapi, hakukuwa na majibu na hivyo madiwani kutoridhishwa na hilo huku wakitaka wananchi hao kuungana pamoja kwa ajili ya kufuatilia suala hilo.

Dk. Slaa aliitaka serikali kuangalia suala la kujenda viwanda vya ndani kusaidia wazalendo badala ya kuwaondoa kwenye maeneo kama hayo ambayo wanaendesha shughuli zao kwa ajili ya masuala ya kiuchumi na ajira zao.

MAMBO YAKE; WEMA AMTAMBULISHA MSANII MPYA WA KAMPUNI YAKE

Wema Sepetu, akiwashukuru mashabiki zake kwa sapoti waliyompa kwa mwaka 2014 na kumtambulisha msanii Luna.

Msanii wa Bongo Fleva, Ally Luna (kushoto), akiimba wimbo es kumsifia Wema mara baada ya kutambulishwa kuwa chini ya Kampuni ya Endless Fame. 


Wema Sepetu akimtunza Luna.

Bob Junior akikamua jukwaani.

Msanii wa Bongo Fleva, Linex, akiimba huku shabiki yake akizungusha nyonga baada ya kuguswa na moja ya nyimbo zake.

Barnaba Boy akitumbuiza.

Mmoja wa mashabiki waliohudhuria ndani ya Club 71 akicheza na Barnaba Boy.

Mwigizaji wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel, akizama ndani ya Club 71 na marafiki zake.

Msanii aliye chini ya Kampuni ya Endless Fame, Mirra, akikamua.

Mmoja wa mabaunsa wa ukumbi huo akimuondoa jukwaani mrembo mmoja baada ya kuguswa na wimbo wa Mirra na kuamua kulivamia jukwaa.


Msanii wa Hip Hop, Izzo Business, akipagawisha mashabiki.

Godzilah akitoa burudani.

Mtangazaji wa Clouds FM, Soud Brown, akiwa na keki aliyopewa na Wema Sepetu kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa ambayo ilifanyika usiku huo.

Soud Brown akimlisha kipande cha keki Wema Sepetu.

Mmoja wa mapaparazi wa mtandao huu Musa Mateja (kulia), akilishwa keki na Soud Brown.

Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel, akilishwa keki.

Wema akiselebuka na meneja wake Martine Kadinda.

MKURUGENZI wa kampuni ya Endless Fame, Wema Sepetu, usiku wa kuamkia leo amemtambulisha msanii mpya wa Bongo Fleva, Ally Luna, ambaye takuwa mmoja wa wasanii wa kampuni hiyo na kusimamiwa shughuli zote za kimuziki kama ilivyo kwa mwanamuziki Mirra.

Tukio hili lilifanyika ndani ya Ukumbi wa Club 71 uliopo Tegeta jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa pia na shoo maalum ya kufunga mwaka kwa kampuni hiyo na kuwashukuru wadau wote waliowaunga mkono.
Shoo hiyo ilisindikizwa na wasanii kibao wa Bongo Fleva, wakiwemo Bob Junior, Godzilah, Izzo Business, Barnaba Boy, Linex na Mirra.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...