2015-03-31

VANESSA MDEE ATOBOA SIRI NZITO!!............soma hapa kujua alichokisema


VANESSA Mdee ambaye ameutambulisha rasmi wimbo wake mpya wa ‘No body but me’, ameweka wazi kwamba kushindwa kumudu gharama za uandaaji wa video, muziki bora kumekuwa sababu kubwa kwa wasanii wa kike kujiingiza katika mapenzi na watayarishaji wa muziki. 

Vanessa alitoa siri hiyo juzi alipotembelea ofisi za New Habari (2006) Ltd inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, Rai na The African. 

Alisema wasanii wengi wa kike wanajikuta wanahitaji fedha kwa ajili ya kugharamia vitu vingi studio, video zao na gharama za mahitaji kwa ajili ya video bora lakini wanaposhindwa baadhi yao hujikuta wakinasa kimapenzi na maprodyuza ama watakaowagharamia. 

“Sijawahi kukutana na ushawishi wa kunitaka kimapenzi kwa sababu ninaweza kujigharamia kila kitu wakati ninapoandaa nyimbo zangu, lakini ni kweli wasanii wengi wa kike wasiokuwa na fedha ya kutosha wanajiingiza katika mapenzi baada ya kupungukiwa fedha,” alisema. 

Msanii huyo alisema alianza kujiandaa kuwa msanii mkubwa tangu akiwa shuleni kwa kujifunza kuimba, kucheza pamoja na kutumia vifaa vya muziki wakati familia yake ilipokuwa ikimuandalia vyanzo vya mapato kwa ajili ya muziki wake.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...