2014-10-27

MTANZANIA NJE, BBA






Matumaini ya watu wengi kumuona mshiriki kutoka Afrika Mashariki ndani ya jumba la Big Brother Africa kuibuka na ushindi, yameshuka kwa kiasi kikubwa baada ya washiriki kutoka nchi mbili za Afrika Mashariki kutolewa nje ya jumba hilo.

Aliekuwa mshiriki wa Tanzania Laveda kwenye Big Brother Hotshots 2014.

Wiki moja baada ya washiriki Lillian kutoka Nigeria, Esther kutoka Uganda na Sabina kutoka Kenya kutolewa kwenye mjengo huo, Mtanzania Laveda aliyekuwa na mahusiano ya karibu na Permithias pamoja na Mkenya Alusa wamekutana na ‘rungu’ la kura lililowatupa nje ya jumba hilo.

Laveda anakuwa mshiriki wa sita wa jinsia ya kike kutolewa nje ya jumba la BBA huku Alusa akiwa ni mshiriki wa kwanza wa kiume kutolewa Big Brother Hotshots.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...