Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, jana alimtembea Askofu Gwajima hospitalini hapo kumjulia hali.
Lipumba amekuwa kiongozi wa pili wa kisiasa kufika hospitalini hapo kumjulia hali Gwajima, baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa aliyefika kwa mara ya kwanza Jumamosi na kurudi tena jana.
Profesa Lipumba ambaye hivi karibuni pia aliishiwa nguvu wakati akihojiwa na polisi, alisema kitendo kinachofanywa na jeshi hilo cha kutumia nguvu kinatakiwa kukemewa kwa nguvu zote.
Akizungumza baada ya kumjulia hali Gwajima, alisema yeye ni miongoni mwa waliopatwa na hali hiyo akiwa mikononi mwa polisi kutokana na kuacha kuuliza suala husika na kutishatisha, kusumbua sumbua, kitu kinachomfanya anayehojiwa kujisikia vibaya na hata kupoteza fahamu.
Aliongeza kwamba kwa kuwa Kardinali Pengo ameshatangaza msamaha kwa Askofu Gwajima, hakuna haja ya kuendelea kumshikilia.
Dk Slaa alisema kinachofanywa na polisi ni upotoshaji na hapingi wala haingilii kinachoendelea kati ya Gwajima na Pengo, bali analaani kitendo cha polisi kupotosha ukweli.
Dk Slaa alisema polisi wanapotosha ukweli kwa kuwaeleza wananchi kitu ambacho hakina ukweli kwa masilahi yao kama ambavyo wamekuwa wakiwafanyia viongozi wa siasa, akiwamo yeye.
Alisema kitendo kilichomkuta Gwajima hata yeye kiliwahi kumkuta .Alikamatwa na bastola aliyoisajili na kuilipia kila kitu, siku iliyofuata polisi wakamtuhumu kuwa ni jambazi anamiliki silaha isivyo halali.
“Mimi nasema waache wawapeleke mahakamani, ukweli utabainika,” alisema Slaa.
“Mimi nasema waache wawapeleke mahakamani, ukweli utabainika,” alisema Slaa.
0 comments:
Post a Comment