2014-11-10

Washiriki Wawili NJE BBA "HotShots"

 
Jana ilikuwa siku ya 35 tangu kuanza msimu wa Big Brother Africa Hot shots ambapo list ya washiriki waliotolewa ndani ya jumba hilo imezidi kuongezeka huku November 9 2014 ikiweka rekodi za kutolewa kwa washiriki wengine wawili kama wiki iliyopita.
 Kama ulikua mbali na TV yako taarifa ikufikie tu kwamba waliotolewa niPermithias kutoka Namibia na Frankie mwakilishi wa Rwanda wametolewa ndani ya jumba hilo na kufanya idadi ya washiriki waliotoka kuwa kumi na mbili, sita wa kike na sita wa kiume.
Wiki iliyopita washiriki watatu walitoka akiwemo Arthur wa Rwanda pia ambapo Frankie anakuwa mshiriki wa pili kutoka nchi ya Rwanda kutolewa BBA.

Frankie mwakilishi wa Rwanda ndani ya Big Brother akiagana na washiriki wenzake.
   
Permithias wa Namibia akiagana na washiriki wenzake BBA.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...