WATU
zaidi ya 25 wajeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea jana baada ya
gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Costa kutoka Mbozi kuelekea
Mbeya kupinduka katika eneo la Senjele wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya.
Ajali
hiyo ilihusisha gari aina ya Costa lenye namba za usajili T 336 CJY
ambalo lilipinduka baada ya kumshinda dereva wakati akijaribu kulikwepa
gari lingine aina ya Suzuki lenye namba za usajili T 327 ARZ.
Kwa
mujibu wa baadhi ya majeruhi walionusurika kwenye ajali hiyo walisema
chanzo ni dereva kushindwa kulimudu gari la abiria baada ya kulikwepa
gari dogo kutokana na kuwa na mwendokasi pamoja na mvua kubwa iliyokuwa
ikiendelea kunyesha.
Baadhi
ya majeruhi walikimbizwa katika Hospitali teule ya Ifisi na wengine
wakipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibabu
zaidi.
|
0 comments:
Post a Comment