2015-03-23

JINI KABULA AFAKAMIA ‘MIKUKU’ UWANJANI!



Uroho? Mwigizaji wa sinema za Kibongo aliyeibuliwa na mchezo wa runingani wa Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ juzikati alinaswa akifakamia minofu ya kuku katika ya kadamnasi iliyojitokeza katika Dimba la Taifa jijini Dar.

Tukio hilo lilinaswa na Ijumaa Wikienda, Machi 17, mwaka huu ndani ya uwanja ambapo kulikuwa na mtanange kati ya Yanga na Kagera Sugar.

Akiwa uwanjani hapo muda mfupi kabla ya mechi kuanza, Jini Kabula alishuhudiwa akifakamia ‘mikuku’ na rafiki zake, jambo lililowafanya baadhi ya mashabiki wanaomfahamu kumkodolea macho muda mwingi.

Pamoja na hali hiyo, Kabula hakuonekana kujali chochote akaendelea kutafuna kuku kwa fujo na hata mwanahabari wetu alipomhoji juu ya upatikanaji wa kuku hao ndani ya uwanja huo, staa huyo alisema kuwa aliwanunua nje ya uwanja hivyo hata kula katikati ya watu haoni noma.

“Acha nile kwa raha zangu, mimi nina njaa na ndiyo maana nilipitia kuku wangu nje ya uwanja na kuja nao hapa,” alisema Kabula.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...